Posts

MLIPUKO WAUA WAWILI BAGAMOYO

Image
  Watu wawili wamefariki dunia na mmoja kujeruhiwa baada ya kutokea mlipuko ambao bado haujafahamika ni wa kitu gani. Akitoa Taarifa kwa vyombo vya habari, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Salim Morcase, amesema tukio hilo limetokea leo tarehe 31 Agosti 2025 Mtaa wa kichemchem kata ya Nianjema wilayani Bagamoyo majira ya saa moja na dakika ishirini asubui. Amesema chanzo cha vifo hivyo ni mlipuko wa chuma ambacho Doto Mrisho (Marehemu) alikuwa anakikata kwenye karakana yake ya kuchomelea mageti. Waliofariki katika tukio hilo ni Doto Mrisho mwenye umri wa miaka 24 fundi wa kuchomelea mageti mkazi wa kichemchem kata ya Nianjema na Saidi Ramadhani mwenye umri wa miaka 53 mkazi wa Sanzale Bagamoyo, na aliyejeruhuwa katika tukio hilo ni  Hassan Omari, mkazi wa Sanzale Bagamoyo. Kamanda Morcase amesema uchunguzi wa tukio hilo unaendelea kufanyika na jeshi la polisi kwa kushirikiana na vyombo vingine vya usalama ili kubaini chanzo cha mlipuko huo na ...

MARIAN SCHOOLS MARATHON NI KESHO

Image
  Na Albert Thomas Kawogo. TAASISI ya Marian Schools Bagamoyo imeandaa mbio za marathon MARIAN SCHOOLS MARATHON 2025 zitakazofanyika Bagamoyo Ijumaa ya tarehe 15  Agosti. Msemaji wa Marian Schools, Ohsana Mnalunde amesema mbio hizo zitaanzia kwenye kijiji cha Zinga Samakisamaki na kumalizikia kwenye hoteli ya Stella Maris Bagamoyo mjini. Mnalunde amesema tayari zaidi ya washiriki 5,000 wamethibitisha ushiriki wao huku idadi kubwa ya watu wa Bagamoyo ikionyesha nia ya kushirki mbio hizo. Msemaji huyo amesema mgawanyo wa mbio hizo ni wa km 21, km 10 na km 5 ambapo idadi ya washiriki watarajiwa ni wanafunzi, wazazi,  wafanyakazi, walimu na wakuu wa mashrika ya serikali na binafsi pamoja na wafanyakazi wao. Naye Meneja wa Taasisi za Marian Schools Padre Valentine Bayo amewataka watu wengi kujitokeza kujisajili ili waweze kushiriki kwani kukimbia ni afya na  kunasaidia kupunguza kasi ya magonjwa yasiyoambukiza (NCDs) kama shinikizo la damu sukari na moyo ambayo huchangia ...

TBN YAKEMEA 'MANABII' WA MITANDAONI, KWA UTABIRI WAO UNAOLETA TAHARUKI KWA JAMII.

Image
  Mkuu wa Mawasiliano Serikalini, Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi, (PDPC) Innocent Mungy, akizungumza katika mafunzo hayo. Na Mwandishi wetu, Dar es salaam. Mtandao wa Bloga Tanzania (TBN) umekemea vikali tabia inayoshamiri ya watu kujinadi kufanya utabiri kwa watu na taifa kupitia mitandao ya kijamii, ukisema vitendo hivyo vinakiuka Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi. Kauli hiyo imetolewa kama azimio katika kikao kazi cha mafunzo ya mabloga kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2025. Mabloga hao wameitaka Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) na Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi (PDPC) kushirikiana kuwasaka na kuwachukulia hatua kali wale wote wanaohusika na vitendo hivyo. Katika kikao hicho, mabloga walibainisha kuwa kumeibuka kundi la watu wanaodai kuwa ni manabii na kutoa kauli zinazokiuka sheria za nchi na kuleta taharuki kuelekea uchaguzi mkuu. Wakitolea mfano wa kauli hizo ni kama vile kusema kutatokea kifo cha kiongozi mkubwa siku za hivi karibuni, au kutatokea machafuko ful...

TCRA YAWAFUNDA BLOGA KUELEKEA UCHAGUZI MKUU 2025

Image
  Na Mwandishi Wetu Wazalishaji wa Maudhui Mtandaoni, wameaswa kutotoa taarifa ambazo zitaleta taharuki na machafuko ndani ya nchi hasa katika kuelekea kipindi cha Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge  na Madiwani  utakao fanyika baadaye mwaka huu (2025). Yamesemwa hayo jana tarehe 3, Agosti 2025 na Meneja Kitengo cha Huduma za Utangazaji,TCRA, Injinia Andrew Kisaka wakati  akiwasilisha makala (mada) katika mkutano ulioandaliwa na  wa  Tume Huru ya Uchaguzi nchini (INEC) kwa  watoa maudhui mtandaoni, amesema kuwa wakati wa uchaguzi kuna mazingira ya migawanyiko, mivutano ya kijamii, na upotoshaji wa hali ya juu hivyo ni muhimu  Mabloga waepuke  kuepuka kusambaza uvumi, kuripoti kwa umakini, kutopendelea upande wowote  na kukemea lugha za chuki. Kisaka amewataka  bloga nchini kote  kuimarisha maadili yao na kuchukua jukumu muhimu katika kuhakikisha uchaguzi unafanyika kwa amani kwa kupandisha maudhui yenye tija na kama unaona maud...

WAZALISHAJI WA MAUDHUI MTANDAONI WAHIMIZWA KUHAMASISHA WANANCHI KUSHIRIKI UCHAGUZI MKUU 2025

Image
Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Mahakama ya Rufani Jacobs Mwambegele akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutanio wa Tume na Wazalishaji Maudhui Mtandaoni kuhusu uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025. Kikao hicho cha siku moja kilifanyika jijini Dar es Salaam leo Agosti 03 , 2025.   Baadhi ya wawakilishi wa serikali waliohudhuria mkutano huo. Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Ndg.Kailima Ramadhani akitoa mada wakati wa ufunguzim wa mkutanio wa Tume na Wazalishaji Maudhui Mtandaoni kuhusu uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025. Kikao hicho cha siku moja kilifanyika jijini Dar es Salaam leo Agosti 03 , 2025. Picha ya pamoja ya washiriki  NA WAANDISHI WETU, DAR ES SALAAM . Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Mahakama ya Rufaa Jacobs Mwambegele, amewahimiza wazalishaji wa maudhui mtandaoni kutumia majukwaa yao ya kidijitali kuhamasisha wananchi kujitokeza kwa wingi kupiga kura katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025. Akizungumza leo...

DIRA 2050 INA KINGA YA BUNGE -PROF MKUMBO

Image
  Na Mwandishi wetu  SERIKALI imewatoa hofu Watanzania kuhusu hoja ya kuwa utekelezaji Dira 2050 unaweza kukumbwa na changamoto ya uhalali wa kisheria na hivyo mpango huo muhimu kwa taifa ukawa na ombwe la kiufanisi hapo baadae  Akiongea katika kikao maalum na Wahariri kutoka jukwaa la Wahariri Tanzania TEF Waziri wa nchi ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaii Profesa Kitila Mkumbo amesema Dira ya taifa 2050 imewekewa ulinzi kwa kupelekwa bungeni na kwamba hakuna Rais atakayeweza kwenda kinyume na uamuzi huo Profesa Mkumbo amesema Dira 2050 itatekelezwa na Marais watatu,na kwa atakaetaka kuibadilisha atatakiwa kupeleka bungeni na kwamba Dira hii imekuwa tofauti kwa kuwa ya 2025 iliishia hatua ya kuidhinishwa na Baraza la Mawaziri tu. Waziri huyo amesema mchakato wa kutengeneza Dira 2050 umepitia hatua 13 ambazo ni kuandaa na kuidhinisha miongozo ya Dira. Mkakati wa kuandika Dira ulianza Aprili mwaka 2023, kwa kuunda vyombo vya kutathimini mchakato wa Dira na kufanya tathimini...

ANUSURIKA KIFO BAADA YA KUPIGWA NA WAFUGAJI.

Image
  Na Omary Mngindo,u ELIAS Madinga mkazi wa Kitongoji cha Mlelani, Kijiji cha Visezi Kata ya Vigwaza Halmashauri ya Chalinze Wilaya ya Bagamoyo Mkoa wa Pwani, amenusurika kifo baada ya kushambuliwa na Wafugaji. Mkazi huyo akiwa na mkewe katika nyumba ya bosi wake Kitongojini hapo, siku ya tukio akipulizia dawa mazao aliona makundi ya ng'ombe yaliyogawanyika mara tatu yakiingia ndani ya shamba hilo. Alisema kuwa alipoona hivyo alianza kuiswaga ili itoke shambani, wakati huo akiwepo kijana mdogo jamii ya Wafugaji na kwamba wakati akiendelea na zoezi ilo ghafla yule kijana alitoweka. "Kwakuwa nilikuwa na zoezi la kupulizia dawa, nikachukua baskeli nikaenda kisimani kuchota maji, wakati narudi nikamuona mke wangu amembeba mtoto wetu wa miezi mitatu wamemzingirwa na Wafugaji hao", alisema Madinga. Aliongeza kuwa"Nikiwa nakaribia aliniambia nisifike kwani ameshashambuliwa na Wafugaji hao, sikumuelewa wakati nikaribia nikajikuta mimezingrwa na kundi la Wafugaji wakaanza kun...