Posts

WMA WATAKA WAKULIMA KUZINGATIA VIPIMO KWENYE UJAZO WA MAZAO.

Image
  Wakala wa Vipimo (WMA) umewataka wakulima kuzingatie sheria ya vipimo inayotaka ujazo wa mazao yao kwenye gunia yasizidi kilo 100. Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Ufundi wa WMA, Albogast Kajungu amefafanua sheria hiyo wakati akizungumza na waandishi wa habari katika manda la WMA kwenye maonesho la wakulima nane nane. Amesema moja ya mambo wanayowaeleza wakulima ni namna ya kuweka ujazo wa mazao yao na kuzingatia vipimo vilivyowekwa na Serikali. Amesema katika kutafsiri neno lumbesa kwenye ujazo wa gunia sheria inasema lumbesa ni kile kilichozidi juu ya ujazo wa kilo 100. Ameongeza kwa kusema kuwa wakulima wanapaswa kuzingatia sheria ya ujazo wa mazao kwenye gunia nayo ni kuhakikisha ujazo huo usizidi kilo 100. Amesema sheria inataka mazao yote yanapaswa yafungashwe kwenye ujazo wa kilo 100 na si vinginevyo. Katika kuhakikisha sheria hiyo inatekelezwa ili kulinda haki ya mkulima na mnunuzi, inashauriwa kuwe na vituo vya kuuzia mazao ambapo mizani itawekwa hapo ili kuhakiki ujazo maz...

WANASHERIA WATATUA MIGOGORO ZIARA YA RAIS SAMIA MOROGORO

Image
  Na Mwandishi Wetu TIMU ya wanasheria wa kampeni ya Mama Samia Legal Aid imeambatana na Rais Samia Suluhu Hassan kwenye ziara yake ya mkoani Morogoro kwaajili ya kusikiliza na kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili wananchi. Rais Samia yuko katika ziara ya siku sita mkoani Morogoro iliyoanza tarehe mbili na inayotarajiwa kukamilika tarehe saba siku ya Jumatano mwezi huu. Akizungumza na mwandishi wa habari hii jana, Mkurugenzi Msaidizi wa Ufuatiliaji Haki wa Wizara ya Katiba na Sheria, Beatrice Mpembo alisema wameambatana na Rais Samia ili kusikiliza na kutatua changamoto za wananchi wanaohitaji msaada wa kisheria. “Tutakuwa na Rais muda wote wa ziara hapa Morogoro na tupo na Waziri wetu mheshimiwa Pindi Chana na wasaidizi wa kisheria ngazi ya wilaya na mkoa, kila anapofika mheshimiwa Rais kama kuna mtu anachangamoto ya kisheria tunaichukua na kuifanyia kazi,” alisema “Kupitia ziara hii tumeshatoa msaada wa kisheria kwa wananchi mbalimbali na hata jamii ya wamasai tumekutana ...

MAGAZETI YA LEO TAREHE 29JULAI 2024

Image
 

SWEETBERT NKUBA AAHIDI KULETA MABADILIKO TLS.

Image
  Na Mwandishi Wetu Mgombea wa urais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), Sweetbert Nkuba ameelezea namna ambavyo amejipanga kuleta mabadiliko ndani ya chama hicho endapo atachaguliwa kushika nafasi hiyo. Moja ya mipango yake amesema ni kuboresha miundombinu ya TLS, uimarishaji wa miundombinu ya kisheria na kiteknolojia ili kuwezesha huduma bora kwa wanachama na jamii hususani kuongeza uwekezaji katika mifumo ya kidijitali ya kurahisisha upatikanaji wa taarifa na huduma za kisheria na kuboresha ofisi za TLS katika mikoa mbalimbali kwa vifaa vya kisasa na miundombinu bora. Jambo la pili anasema atasisitiza mafunzo endelevu kwa wanachama wa TLS ili kuhakikisha kuwa wanasheria wanakuwa na ujuzi wa kisasa na uwezo wa kushindana kimataifa ikijumuisha kuanzisha programu za mafunzo ya mara kwa mara kuhusu sheria mpya na mabadiliko ya sheria pamoja na kushirikiana na taasisi za kimataifa kwa mafunzo na kubadilishana uzoefu. La tatu anasema atahakikisha TLS inakuwa na sauti yenye nguvu...

KATIBU MKUU CCM, DKT NCHIMBI AZURU KABURI LA HAYATI MKAPA.

Image
  CCM YATOA MILIONI 10 KUBORESHA MAJENGO YA SHULE LUPASO Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi ametembelea kaburi la aliyekuwa Rais wa Awamu ya 3, hayati Benjamin William Mkapa katika Kijiji cha Lupaso mkoani Mtwara, leo Julai 28, 2024, kuhani familia na kuzungumza na wananchi wa Lupaso. Balozi Nchimbi amesema “naomba nikiri kuwa mimi ni mwanafunzi wa hayati na nimekuwa Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana Taifa (UVCCM), katika kipindi chake, ndiye alinilipia ada ya kusoma chuo kikuu na alikuwa mfuatiliaji sana na alitulea vizuri, sio sisi tu, bali Watanzania wote aliwalea pia. Alikuwa mzalendo kwa nchi, alifanya mabadiliko makubwa kwa nchi yake na kwa Chama chake, lakini yote CCM chini ya Dkt Samia tutaendelea kuyaenzi yale yote aliyoyoacha hayati Benjamin Mkapa.  Pamoja hayo nimeambiwa kero za hapa na tumezichukua. CCM inatoa shilingi milioni 10 kuanza kukarabati shule ya hapa Lupaso.” Katika ziara hii Dk Nchimbi ameambatana na Katibu wa NEC-Itikadi, ...