TANZANIA KUWA MWENYEJI MKUTANO WA KIMATAIFA WA BARABARA.
Na Mwandishi Wetu TANZANIA inatarajiwa kuwa mwenyeji wa Kongamano la tisa la Kimataifa la Usafiri Endelevu na Ubunifu Bora ambao umeandaliwa na Chama cha Wataalamu wa Barabara (TARA). Mkutano huo utakaofanyika jijini Arusha wiki ijayo utafunguliwa na Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa na utahudhuriwa na washiriki zaidi ya 300 wa ndani na nje ya nchi. Mkurugenzi Mkuu wa TARA, Eliamlisi Joseph, alisema jana kuwa mada kuu ya kongamano hilo itakuwa Usalama, Umakini na Uendelevu wa Mifumo ya Usafiri kwa Ukuaji wa Uchumi Duniani. Alisema madhumuni ya mkutano huo wa Kimataifa wa usafiri endelevu na ubunifu bora ni kuwajengea uwezo wadau wa sekta ya usafiri kuhusu usafiri salama, mahiri na endelevu na mifumo ya ukuaji wa uchumi ulimwenguni kupitia kubadilishana maarifa, uzoefu na mbinu bora. Alisema lengo ni kuwawezesha wadau katika sekta ya uchukuzi, kuchangia ipasavyo katika maendeleo, utekelezaji na usimamizi wa mifumo endelevu na bora ya usafiri na kutoa jukwaa la...