Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Mhe. Halima Okash tarehe 20 Julai, 2024 amewasilisha taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya CCM mbele ya Halmashauri Kuu ya CCM Wilaya ya Bagamoyo kuanzia Januari hadi Juni 2024 katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze.
Akiwasilisha taarifa hiyo mkuu huyo wa wulaya, alisema kuwa, kwa ujumla Halmashauri zote mbili zimeendelea kufanya vizuri katika nyanja zote hasa upande wa ukusanyaji wa mapato, miundombinu ya Elimu na Afya.
"Waheshimiwa wajumbe kwa upande wa ukusanyaji mapato mfano Halmashauri ya Wilaya Bagamoyo kwa Mwaka wa fedha 2023/24 ilipanga kukusanya bilion 5.8 lakini kwa ujumla imefanikiwa kukusanya Sh bilioni 6.3 sawa na aslimia 106 haya ni mafanikio makubwa.Alisema Mhe. Okash.
Hata hivyo,Mhe Okash alimshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kuwapatia Fedha za ujenzi wa miradi ya maendeleo pamoja na uboreshaji wa huduma za afya, maji na umeme.
Halmashaurji Kuu ya CCM Wilaya ya Bagamoyo iliridhishwa na utekelezaji wa Ilani ya CCM kwa kipindi cha kuanzia January hadi June 2024.
No comments:
Post a Comment