Posts

TANZANIA KUWA MWENYEJI MKUTANO WA KIMATAIFA WA BARABARA.

Image
  Na Mwandishi Wetu TANZANIA inatarajiwa kuwa mwenyeji wa Kongamano la tisa la Kimataifa la Usafiri Endelevu na Ubunifu Bora ambao umeandaliwa na Chama cha Wataalamu wa Barabara (TARA). Mkutano huo utakaofanyika jijini Arusha wiki ijayo utafunguliwa na Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa na utahudhuriwa na washiriki zaidi ya 300 wa ndani na  nje ya nchi. Mkurugenzi Mkuu wa TARA, Eliamlisi Joseph, alisema jana kuwa mada kuu ya kongamano hilo itakuwa  Usalama, Umakini na Uendelevu wa Mifumo ya Usafiri kwa Ukuaji wa Uchumi Duniani. Alisema madhumuni ya mkutano  huo wa Kimataifa wa usafiri endelevu na ubunifu bora ni kuwajengea uwezo wadau wa sekta ya usafiri kuhusu usafiri salama, mahiri na endelevu na mifumo ya ukuaji wa uchumi ulimwenguni kupitia kubadilishana maarifa, uzoefu na mbinu bora. Alisema lengo ni kuwawezesha wadau katika sekta ya uchukuzi, kuchangia ipasavyo katika maendeleo, utekelezaji na usimamizi wa mifumo endelevu na bora ya usafiri na kutoa jukwaa la...

WANANCHI WATAKIWA KUJITOKEZA UBORESHAJI DAFTARI LA WAPIGA KURA

Image
  Na Alodia Dominick  Bukoba, Wadau mbalimbali  wa uchaguzi hapa nchini wameombwa kuhamasisha jamii kujitokeza wakati wa uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura.  Wito huo umetolewa Julai 24, 2024 na mwenyekiti wa tume huru ya taifa ya  uchaguzi Jaji Mbarouk S Mbarouk katika mkutano wa tume na wadau wa uchaguzi mkoani Kagera ambao ulilenga kutoa taarifa  mbalimbali za maandalizi ya uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura. Amesema kuwa, uzinduzi la daftari la kudumu ulifanyika mkoani Kigoma na Waziri  mkuu wa Tanzania Kasimu Majaliwa na kuwa uzinduzi awamu ya pili utafanyika kuanzia Agosti  05, mwaka huu hadi Agosti 11, mwaka huu katika mikoa ya Kagera na Geita. Amewaomba viongozi wa dini, makundi mbalimbali ya wenye ulemavu na wanawake kuhamasisha wananchi kujitokeza kupiga kura na akasema mama  wajawazito, wenye watoto wachanga, wazee na wenye ulemavu watapewa kipaumbele wakati wa kupiga kura.  Wakati huo huo, Kaimu mkurug...

MAONYESHO YA VYUO VIKUU 15 NJE YA NCHI KUFANYIKA ARUSHA

Image
  Na Mwandishi Wetu   VYUO 15 kutoka nje ya nchi vinatarajiwa kushiriki maonyesho yanayotarajiwa kufanyika siku ya Jumamosi jijini Arusha. Maonyesho hayo ya siku moja yatafanyika siku ya Jumamosi tarehe 27 mwezi huu, kwenye hoteli ya Four point by Sheraton Hoteli, zamani ikijulikana kama New Arusha. Mkurugenzi wa Global Education Link (GEL), Abdulmalik Mollel, alisema walianza kufanya maonyesho Zanzibar kuanzia tarehe 15 hadi 21 mwezi huu na mahitaji yamekuwa makubwa kwa wanafunzi. Alisema baada ya kumaliza maonyesho ya Zanzibar GEL ilifanya maonyesho mengine jijini Dar es Salaam lakini kutokana na mahitaji kuwa makubwa kwenye mikoa mingine wameandaa mengine jijini Arusha. “Maonyesho ya Zanzibar yalifana sana na wanafunzi wamekuwa wengi kwa hiyo tulipoona mahitaji yamekuwa makubwa tumeona tufanye na Arusha siku ya Jumamosi ili wanafunzi wengi  wapate fursa ya masomo,” alisema. Alisema mwanafunzi atakayeshiriki kwenye maonyesho hayo atapata taarifa zote kuhusu vyuo vikuu n...

CTI WADAU WA VIWANDA WATETA KUHUSU DIRA YA TAIFA 2050.

Image
  Na Mwandishi Wetu SHIRIKISHO la Wenye Viwanda (CTI), limependekeza maendeleo ya viwanda yapewe kipaumbele kwenye Dira ya Taifa ya 2050.   Hayo yamesemwa leo jijini Dar es Salaam na Mwenyekiti wa CTI, Leodegar Tenga wakati wa mjadala wa wadau wa viwanda wakijadili Dira ya 2050 na kuzungumzia maendeleo ya viwanda kwa ujumla.   Mkutano huo ulioandaliwa na Shirikisho la Wenye Viwanda (CTI), pia ulizindua tuzo za Rais za Mzalishaji Bora Viwandani PMAYA ambazo hufanyika kila mwaka kwa wenye viwanda.   Tenga alisema hakuna  nchi duniani hata moja ambayo iliwahi kupiga hatua kubwa kiuchumi bila kuwekeza kwenye viwanda kwa hiyo lazima kuwe na mikakati madhubutu ya kukuza viwanda.   “Kuna msemo wa Kiswahili kwamba kupanga ni kuchagua kwa hiyo tuchague kuwekeza kwenye viwanda ili tusonge mbele na ili viwanda vifanye kazi vizuri lazima tuwe na watalamu wetu kwa hiyo tena lazima tuwekeze kwenye elimu bora,” alisema Tenga   Alisema ili viwanda viweze kufanya kazi ...

RAIS DKT. SAMIA AFANYA UTEUZI NA KUHAMISHA NA KUTENGUA BAADHI YA VIONGOZI.

Image
 

DC OKASH AWASILISHA TAARIFA YA UTEKELEZAJI WA ILANI YA CCM BAGAMOYO.

Image
  Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Mhe. Halima Okash tarehe 20 Julai, 2024 amewasilisha taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya CCM mbele ya Halmashauri Kuu  ya CCM Wilaya ya Bagamoyo kuanzia Januari hadi Juni 2024 katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze.  Akiwasilisha taarifa hiyo mkuu huyo wa wulaya, alisema kuwa, kwa ujumla Halmashauri zote mbili  zimeendelea kufanya vizuri katika nyanja zote hasa upande wa ukusanyaji wa mapato, miundombinu ya Elimu na Afya.  "Waheshimiwa wajumbe kwa upande wa ukusanyaji mapato mfano Halmashauri ya Wilaya Bagamoyo kwa Mwaka wa fedha 2023/24 ilipanga kukusanya bilion 5.8 lakini kwa ujumla imefanikiwa kukusanya Sh bilioni 6.3 sawa na aslimia 106 haya ni mafanikio  makubwa.Alisema Mhe. Okash.  Hata hivyo,Mhe Okash alimshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa wa Tanzania Dkt. Samia  Suluhu Hassan kuwapatia Fedha za ujenzi wa miradi ya maendeleo pamoja na uboreshaji wa huduma za afya, maji na umeme.  Halmashaurji...

GLOBAL EDUCATION LINK YADAHILI WANAFUNZI MAONYESHO YA VYUO VIKUU ZANZIBAR.

Image
  Na Mwandishi Wetu WAKALA wa Elimu ya Vyuo Vikuu nje ya Nchi Global Education Link (GEL), imeanza kudahili wanafunzi papo hapo kwenye maonyesho yanayoendelea kwenye viwanja vya Maisala visiwani Zanzibar. Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa GEL, Abdulimalick Mollel, wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu maonyesho hayo yanayoendelea visiwani humo. Alisema kwenye maonyesho hayo kuna vyuo vya nje ya nchi ambavyo vimetoa udhamini wa asilimia 50 kwa wanafunzi wanaotaka kwenda kusoma kwenye vyuo hivyo na vingine vimetoa ufadhili wa asilimia 100. “Tumeleta wawakilishi wa vyuo 20 kutoka Irani kuna ufadhili wa asilimia 100 analipiwa kila kitu na kuna vyuo ambavyo mwanafunzi atalipiwa asilimia 50 ya ada kwa hiyo mwanafunzi akija kwenye maonyesho haya akichagua kozi GEL tunamdahili hapahapa,” alisema Alisema lingine la manufaa kwenye maonyesho hayo ni uhusiano wa vyuo vikuu vya ndani na nje ya nchi kwani uzoefu unaonyesha kuwa asilimia kubwa ya wahitimu wa vyuo vya nje ya nchi wanaajir...