Posts

BARAZA LA MADIWANI LAPITISHA BAJETI YA BILIONI 38.9 KWA MWAKA WA FEDHA 2024/25

Image
  Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo limepokea na kupitisha bajeti ya shilingi Bilioni 38,982,000,000.00 kwa mwaka wa fedha 2024/2025 huku shilingi Bilioni 6,482,058,127.00 ikitarajiwa kukusanywa katika mapato ya ndani na shilingi 32,496,016,000.00 ruzuku kutoka Serikali kuu. Bajeti hiyo imepitishwa Tarehe 30 Januari 2024 katika kikao maalumu cha Baraza la Madiwani kilichofanyika katika ukumbi wa Halmashauri hiyo. Akiwasilisha bajeti hiyo, Mjumbe wa Kamati ya Fedha, Uongozi na Mipango, ambae pia ni Diwani wa Kata ya Nianjema, Abdul Pyallah amesema ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji isimamie kikamilifu mikakati ya ukusanyaji mapato. Akizungumza katika Baraza hilo, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Bagamoyo, Mhe. Mohamed Usinga, amemtaka Mkurugemzi kuwachukulia hatua kali za kinidhamu wakuu wa idara ambao watakamilisha miradi huku ikiwa na madeni. Usinga alisema ipo tabia ya baadhi ya wakuu wa idara kutekeleza Miradi huku wakiwa wanakopa kwa wazabuni na kuisababishia Ha...

TAKUKURU KAGERA YAWANOA WAANDISHI KUELEKEA UCHAGUZI SERIKALI ZA MITAA.

Image
  Na Alodia Babara Bukoba Mkuu wa Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa TAKUKURU mkoa wa Kagera amewasihi waandishi wa habari mkoani humo kutoa ushirikiano kwa taasisi hiyo katika kuelimisha jamii na kufichua vitendo vya rushwa kuelekea uchaguzi wa Serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika mwaka huu. Mkuu huyo Pilly Mwakasege aliyasema hayo Januari 30, mwaka huu wakati akifungua mafunzo ya siku moja yaliyotolewa na taasisi hiyo kwa waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali mkoani Kagera ambapo amesema kuwa, wanawategemea waandishi wa habari kuwapa ushirikiano katika kuwapatia taarifa mbalimbali zinazohusu vitendo vya rushwa kwa sababu ni watu muhimu katika jamii na wanauwezo wa kufika kokote na wanaaminiwa sana na jamii. Amesema kuwa, vyombo vya habari vikitumika vizuri vitaleta mabadiliko kwa jamii kwani watapatikana  viongozi bora na si bora viongozi ambao watasimamia vizuri miradi ya maendeleo na kukemea viashiria vya rushwa. Amewasisitiza waandishi wa habari kutumia...

KILIMO SHADIDI CHA MPUNGA CHAANZA KUCHANGAMKIWA.

Image
Na Mwandishi wetu- Mbeya. Wakulima wa zao la mpunga wameeleza kufurahishwa na Mfumo wa Kilimo Shadidi cha Mpunga,  chenye kuhimili athari za mabadiliko ya tabia nchi kwa kutumia mfumo wa kuongeza mpunga (SRI) ambao unapunguza  gharama za uzalishaji huku tija ikiwa inaongezeka  mara dufu ya kilimo cha kawaida. Hayo yameelezwa  katika kikao Cha mwaka cha Wadau wa Kilimo shadidi kilichofanyika Januari 24-27 Jijini Mbeya katika viunga vya Kituo Cha Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania TARI Uyole. Akielezea hili, Mkulima wa Skimu ya Mkula Wilaya ya kilombero Mkoani Morogoro Filbert Kadebe, amesema katika Kilimo cha kawaida alikuwa akipanda mbegu kilogramu 30 kwa hekari moja lakini kwa kutumia  Mfumo wa Kilimo Shadidi cha Mpunga  wenye kanuni ya kutumia kitalu mkeka anapanda mbegu kilogramu 2 hadi 3 kwa hekari moja. Pia, Kadebe alisema upandaji wa mche mmoja katika kilimo shadidi unatoa machipukizi mengi ambayo hupelekea kuongezeka kwa mavuno ukilinganisha na u...

BARAZA LA WAFANYAKAZI BAGAMOYO, LAPITISHA BAJETI YA BILIONI 38.9 

Image
  Na Hamisi Hamisi, Zuhura Kassimu.Bagamoyo Baraza la wafanyakazi la Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo limepitisha bajeti ya Shilingi Bilioni 38,978,074,127.00 kwa mwaka wa fedha 2024/2025 huku shilingi bilioni 6,482,058,127.00 ikitarajiwa kukusanywa katika mapato ya ndani ya Halmashauri na shilingi Bilioni 32,496,016,000.00 ruzuku kutoka serikali kuu. Bajeti hiyo imepitishwa januari 25,2024 katika kikao maalum cha kamati tendaji ya Baraza la wafanyakazi ya Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa halmashauri hiyo.  Aidha, shilingi Bilioni 6,486,058,127.00 kutoka mapato ya ndani kati ya fedha hizo mapato huru ni Bilioni 3,417,946,627.00 na mapato fungiwa ni Bilioni 3,068,111,500.00 na makadirio hayo ni ongezeko la shilingi milioni 593,528,127.00 kutoka kiasi cha shilingi Bilioni 5,892,530,000.04 kilichoidhinishwa kutumika mwaka wa fedha 2023-2024 sawa na ongezeko la asilimia 10%    Akiwasilisha bajeti hiyo, Afisa Mipango wa Ha...

DC OKASH KUWACHUKULIA HATUA WAZAZI WASIOWAPELEKA WATOTO SHULE

Image
  Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Mhe. Halima Okash amesema atawachukulia hatua Kali wazazi wote watakashindwa kuwapeleka watoto shule ifikapo Jumatatu tarehe  15 January,2024. Akizungumza Kwa nyakati tofauti wakati wa ziara ya upokeaji wanafunzi katika Shule mbalimbali Halmashauri ya Bagamoyo alisema kuwa msako mkali utafanyika Kwa wazazi watakaoshindwa kuwapeleka watoto shule. " Niwaambie tu  ndugu zangu tutawashughulikia wazazi wote watakaoshindwa kuwapeleka watoto wao Shule ifikapo Mwisho wa Wiki hii, na Jumatatu tutaanza msako mkali ". Alisema Mhe. Okash

DC OKASH AKEMEA UNYANYASAJI WA KIJINSIA BAGAMOYO.

Image
  Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Mhe.Halima Okash amekemea vikali vitendo vya unyanyasaji wa kijinsia unaendelea katika Wilaya ya Bagamoyo. Akizungumza na wazazi pamoja na waalimu alipotembelea Shule ya Sekondari Nianjema Leo tarehe 10 Januari, 2024 alisema kuwa, kuna ongezeko kubwa la ukatili wa kijinsia katika maeneo mengi ya Bagamoyo ikiongozwa na Kata ya Mapinga pamoja na Nianjema. "Niwaambie tuu kuwa, Mimi kama Mkuu nasikitishwa sana na vitendo vya unyanyasaji wa kijinsia unaoendelea katika maeneo yetu hivyo hatutasita kuwachukulia hatua wahusika wote watakaobanika kujihusisha na vitendo hivyo. Nawaomba wazazi muwe mstari wa mbele kuwalinda watoto wenu".Alisema Mhe. Okash. Aidha Mhe. Okash aliwaomba wazazi kuwapeleka Shule watoto wote waliojiandikisha kuanza madarasa ya awali,la kwanza na kidato Cha Kwanza Kwa Sasa hakuna shida ya watoto kuripoti shuleni kwani Serikali Kwa makusudi imeondoa ada Ili kuhakikisha kuwa watoto wote wanapata Elimu. Aliwashauri walimu na wazaz...

RMO KAGERA ATENGULIWA KWA KUZUILIWA MWILI WA MTOTO MCHANGA KWA MADAI YA DENI LA MATIBABU HOSPITALINI.

Image
  Na Alodia Babara Bukoba. Waziri wa nchi ofisi ya Rais TAMISEMI Mohamed Mchengerwa amemwagiza katibu mkuu wa TAMISEMI nchini kutengua nafasi ya mganga mkuu wa mkoa wa Kagera Issesanda Kaniki baada ya hospitali ya rufaa ya Bukoba ya mkoa huo kuzuia mwili wa mtoto mchanga kwa muda wa siku mbili kutoruhusiwa kwenda kuzikwa wakati wakijua watoto wanatibiwa bure. Maagizo mengine ameyatoa kwa viongozi wa serikali, siasa na watumishi mbalimbali nchini. Waziri Mchengerwa ametoa maagizo hayo  Desemba 15, mwaka huu wa 2023, wakati akizungumza na wananchi wa mkoa wa Kagera katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika kituo cha mabasi yaendayo mikoani kinachokarabatiwa ambapo pia alishuhudia utiaji wa saini ya mikataba ya usanifu miradi ya uboreshaji wa miundomninu ya miji Tanzania (TACTIC) kwa miji 15 ya kundi la pili. Ameagiza katibu mkuu TAMISEMI kwa kushirikiana na sekta ya afya kufanyika mapitio ya menejimenti nzima ya hospitali hiyo na kutoa maamuzi kwani alipata malalamiko ku...