Na Hamisi Hamisi, Zuhura Kassimu.Bagamoyo
Baraza la wafanyakazi la Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo limepitisha bajeti ya Shilingi Bilioni 38,978,074,127.00 kwa mwaka wa fedha 2024/2025 huku shilingi bilioni 6,482,058,127.00 ikitarajiwa kukusanywa katika mapato ya ndani ya Halmashauri na shilingi Bilioni 32,496,016,000.00 ruzuku kutoka serikali kuu.
Bajeti hiyo imepitishwa januari 25,2024 katika kikao maalum cha kamati tendaji ya Baraza la wafanyakazi ya Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa halmashauri hiyo.
Aidha, shilingi Bilioni 6,486,058,127.00 kutoka mapato ya ndani kati ya fedha hizo mapato huru ni Bilioni 3,417,946,627.00 na mapato fungiwa ni Bilioni 3,068,111,500.00 na makadirio hayo ni ongezeko la shilingi milioni 593,528,127.00 kutoka kiasi cha shilingi Bilioni 5,892,530,000.04 kilichoidhinishwa kutumika mwaka wa fedha 2023-2024 sawa na ongezeko la asilimia 10%
Akiwasilisha bajeti hiyo, Afisa Mipango wa Halmashauri ya wilaya Bagamoyo, Bi Huruma Eugene, amesema vipaumbele vimewekwa kupitia fedha za mapato ya ndani ikiwa ni Pamoja na kuongeza ukusanyaji kwa kuanzisha vyanzo vipya, kuimarisha shughuli za usafi na utunzaji wa mazingira katika ngazi zote,kujenga uwezo wa jamii katika masuala ya jamii na kiuchumi kwa kutoa mikopo kwa wajasiliamali wadogo, wanawake ,vijana na walemavu,kuboresha ubora wa elimu kwa kujenga miundombinu katika shule za msingi na sekondari na kuboresha huduma za afya kwa kujenga miundombinu ya vituo vya kutolea huduma za afya.
Akizungumza katika Baraza hilo mmoja wa wajumbe ameiomba Halmashauri kuwa na utaratibu wa kupandisha madaraja kwa watumishi wa kada mbalilimbali Pamoja na kuwalipa stahiki zao kwa wakati. “Naiomba Halmashauri kupitia ongezeko la mapato ya ndani kuhakikisha wanawapandisha watumishi wa kada mbalimbali madaraja pamoja na kuwalipa stahiki zao ili kuongeza weledi katika utendaji kazi’’
Sambamba na hayo wajumbe wamemchagua Ndg .Faraja Mponele kuwa katibu mkuu wa Baraza la wafanyakazi la Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo Pamoja na wajumbe Sita watakaounda kamati tendaji iliyopo chini ya Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Bagamoyo Mhe.Shauri Selenda.
No comments:
Post a Comment