MKUU WA IDARA YA UJENZI KIBAHA MJINI ACHUKULIWA HATUA ZA KINIDHAMU- NDOMBA
Na Mwamvua Mwinyi,Kibaha BARAZA la madiwani Halmashauri ya Mji wa Kibaha ,limemchukulia hatua ya kinidhamu mkuu wa idara ya ujenzi Brighton Kishoa kwa kumkata mshahara wake asilimia 15 ndani ya miaka mitatu , kutokana na uzembe kwenye usimamizi wa ujenzi wa nyumba ya mkurugenzi na kuisababishia hasara Halmashauri hiyo. Hatua hiyo ni fundisho kwa wakuu wa idara na watendaji wengine endapo watazembea na kushindwa kufanya kazi kwa mujibu wa sheria. Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Kibaha,Mussa Ndomba alieleza maazimio hayo katika kikao cha robo mwaka baada agenda iliyojadili makosa ya kinidhamu ya mtumishi huyo ambae amekutwa na makosa ya uzembe na kushindwa kusimamia mradi huo. Alifafanua, kamati za uchunguzi zimefanya kazi yake na kujiridhisha kuwa mkuu huyo wa idara amefanya uzembe. “Hakuna anaependa kuchukuliana hatua kama hizi ,Ila inafikia hatua unachoka kutoa maagizo na kuelekeza kila wakati, adhabu hii anastahili kutokana na makosa aliyopatikana nayo ikiw...