MILIONI 600 KUJENGA SEKONDARI MAKURUNGE BAGAMOYO.
Afisa Elimu Sekondari wa Halmashauri ya Bagamoyo, Aloisi Damian Kaziyareli, (kushoto) na Mtendaji kata Makurunge, Chumi Joel (kulia) wakishiriki katika zoezi la kuchimba msingi kwaajili ya ujenzzi wa shule mpya ya Sekondari inayojengwa kitongoji cha Gezaulole kata ya Mkurunge, Halmashauri ya Bagamoyo, fedha hizo za ujenzi zimetolewa na Rais Samia Suluhu Hassan katika mpango wa kuhakikisha hakuna mtoto aneshindwa kwenda kidato cha kwanza kwa kukosa shule. ................................... Na Athumani Shomari, Bagamoyo. Wanachi wa kata ya Makurunge Halmashauri ya Bagamoyo wamejitokeza kuchimba msingi kwaajili ya ujenzi wa shule mpya ya sekondari inayojengwa kwa fedha zilizotolewa na Rais Samia Suluhu Hassan. Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Bagamoyo, Afisa Elimu Sekondari wa Halmashauri ya Bagamoyo, Aloisi Damian Kaziyareli, amesema ujenzi wa shule hiyo mpya utasaidia kuondoa adha kwa wanafunzi wanaoishi kata ya Makurunge ambao kwa mud...