Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt. Zainab Chaula,akizungumza wakati akifungua kikao na viongozi wa Shirikisho la Umoja wa Wamachinga nchini na viongozi wa Wamachinga kutoka Mikoa 26 nchini kilichofanyika leo Februari 22,2022 jijini Dodoma.
....................................
Na.Alex Sonna, DODOMA
KATIBU Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Dk. Zainabu Chaula amesema mpaka sasa vitambulisho vya wajasiriamali milioni 1.6 vimetolewa nchini kati ya vitambulisho milioni 3.7.
Pia amesema mikakati iliyopo kwa sasa ni jinsi ya kuwapatia vitambulisho vyao wajasiriamali milioni 2.1 waliobaki.
Hayo ameyasema leo Februari 22,2022 Jijini Dodoma wakati akifungua kikao na viongozi wa Shirikisho la Umoja wa Wamachinga nchini na viongozi wa Wamachinga kutoka Mikoa 26 nchini, Dk. Chaula amesema kuwa Januari 25 mwaka huu Rais Samia Suluhu Hassan alikutana na viongozi wa Wamachinga Mkoa wa Dar es salaam ambapo alipokea changamoto na mafanikio wanayokutana nayo.
Amesema kupitia kikao hicho Rais Samia aliagiza kwamba wamachinga ni kundi maalum na sasa liwe chini ya Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum.
Amesema taarifa aliyonayo ni kuwa mpaka sasa vimetolewa vitambulisho milioni 1.6 vya wajasiriamali kati ya vitambulisho milioni 3.7 huku mikakati iliyopo kwa sasa ni jinsi ya kuwapatia vitambulisho vyao wajasiriamali milioni 2.1 waliobaki.
“Lakini taarifa niliyonayo tunawamachinga milioni 3.7 sasa tunataka hawa waliobaki milioni 2.1 tunawapaje vitambulisho sasa ndio maana tunatembea na wenzetu wa TAMISEMI watuambie mchakato unaendaje.Kitambulisho ni jambo jema hata sisi ofisini tuna vitambulisho kwahiyo kitambulisho kinakutambua wewe ni nani na upo wapi lile tutaliboresha,”amesema.
Kuhusiana na kuwatambua wamachinga amesema : “Uzuri mifumo ya Serikali ni endelevu kwahiyo suala la kutambuliwa sio kwamba walikuwa hawatambuliwi,walitambuliwa na walipata usaidizi wote unaostahili isipokuwa kwa sababu imeanzishwa Wizara mpya yenye mambo mahsusi”
Amesema mgawanyo wa shilingi bilioni 5 zilizotolewa na Rais Samia suala hilo Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) linaendelea kulishughulikia
“Ule mgawanyo uliishatolewa kwa ajili ya kuonesha miundombinu na mchakato unaendelea nina imani tukimaliza haya tutajua tunatokaje Tamisemi wataendelea na uratibu,”amesema.
Kwa upande wake,Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo,Amon Mpanju amesema lengo la kikao hicho cha siku mbili ni kulipokea hilo kundi kutoka Tamisemi walikokuwa wakiwahudumiwa mara baada ya Rais kuagiza liwe chini ya Wizara hiyo.
Amesema ndani ya siku mbili watapitishwa katika masuala ya uongozi,taratibu za kiuongozi na namna wanavyoweza kujiongoza kuanzia katika masoko mpaka Taifa,mifumo na mbinu mbalimbali za mawasiliano,pamoja na sheria,taratibu na kanuni za kuongoza umoja wao.
Naye,Mwenyekiti wa Jumuiya ya Machinga nchini Ernest Matondo, amesema kuwa wanakabiliwa na changamoto ya miundombinu katika masoko kutokuwa rafiki ambapo ameomba fedha walizopewa zaidi ya shilingi bilioni 5 ziende kukarabati miundombinu hiyo ili waweze kufanya biashara katika mazingira mazuri.
“Nimpongeze Mheshimniwa Rais kwa kulitambua kundi hili maalum na kutupatia Wizara hili ni jambo la kumshukuru sana Mheshimiwa Rais,”amesema.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Amon Mpanju, akitoa salamu wakati wa kikao na viongozi wa Shirikisho la Umoja wa Wamachinga nchini na viongozi wa Wamachinga kutoka Mikoa 26 nchini kilichofanyika leo Februari 22,2022 jijini Dodoma.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Onesmo Lyanga,akizungumza wakati wa kikao na viongozi wa Shirikisho la Umoja wa Wamachinga nchini na viongozi wa Wamachinga kutoka Mikoa 26 nchini pamoja na Wizara ya Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wanawake na Makundi Maalum kilichofanyika leo Februari 22,2022 jijini Dodoma.
Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Jamii kutoka Wizara ya ya Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wanawake na Makundi Maalum Patrick Golwike,akizungumza wakati wa kikao na viongozi wa Shirikisho la Umoja wa Wamachinga nchini na viongozi wa Wamachinga kutoka Mikoa 26 nchini kilichofanyika leo Februari 22,2022 jijini Dodoma.
Washiriki wa kikao wakifatilia hotuba ya Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt. Zainab Chaula (hayupo pichani) wakati wa kikao na viongozi wa Shirikisho la Umoja wa Wamachinga nchini na viongozi wa Wamachinga kutoka Mikoa 26 nchini kilichofanyika leo Februari 22,2022 jijini Dodoma.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Machinga nchini Ernest Matondo,akitoa neno la shukrani kwa Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt. Zainab Chaula (hayupo pichani) mara baada ya kufungua kikao na viongozi wa Shirikisho la Umoja wa Wamachinga nchini na viongozi wa Wamachinga kutoka Mikoa 26 nchini kilichofanyika leo Februari 22,2022 jijini Dodoma.
Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt. Zainab Chaula akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kufungua kikao na viongozi wa Shirikisho la Umoja wa Wamachinga nchini na viongozi wa Wamachinga kutoka Mikoa 26 nchini kilichofanyika leo Februari 22,2022 jijini Dodoma.
No comments:
Post a Comment