Afisa Elimu Sekondari wa Halmashauri ya Bagamoyo, Aloisi Damian Kaziyareli, (kushoto) na Mtendaji kata Makurunge, Chumi Joel (kulia) wakishiriki katika zoezi la kuchimba msingi kwaajili ya ujenzzi wa shule mpya ya Sekondari inayojengwa kitongoji cha Gezaulole kata ya Mkurunge, Halmashauri ya Bagamoyo, fedha hizo za ujenzi zimetolewa na Rais Samia Suluhu Hassan katika mpango wa kuhakikisha hakuna mtoto aneshindwa kwenda kidato cha kwanza kwa kukosa shule.
...................................
Na Athumani Shomari, Bagamoyo.
Wanachi wa kata ya Makurunge Halmashauri ya Bagamoyo wamejitokeza kuchimba msingi kwaajili ya ujenzi wa shule mpya ya sekondari inayojengwa kwa fedha zilizotolewa na Rais Samia Suluhu Hassan.
Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Bagamoyo, Afisa Elimu Sekondari wa Halmashauri ya Bagamoyo, Aloisi Damian Kaziyareli, amesema ujenzi wa shule hiyo mpya utasaidia kuondoa adha kwa wanafunzi wanaoishi kata ya Makurunge ambao kwa muda mrefu wamekuwa wakitembea umbali wa kilomita zaidi ya kumi kufuata shule ya sekondari.
Ameongeza kuwa, kata hiyo ya Makurunge haikuwahi kuwa na shule ya Sekondari na kwamba ametumia nafasi hiyo kumshukuru Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan kwa kutenga milioni mia sita kwaajili ya ujenzi wa shule hiyo ya sekondari.
Amesema tayari milioni 470 zimeshaingizwa kwaajili ya kazi hiyo ambapo zitatumika kujenga jengo la utawala, vyumba vya madarasa nane, Maabara za sayansi tatu, Maktaba, Vyoo pamoja na nyumba za walimu huku milioni 130 iliyobaki itatolewa baadae.
Afisa elimu huyo amesema kutokana na mpangilio wa majengo hayo, mara tu baada ya kukamilika ujenzi wa shule hiyo itakuwa imejitosheleza na kwamba itakuwa na ubora wa unaotakiwa kwaajili watoto kupata elimu.
Aidha, ametoa wito kwa wazazi kujipanga kusomesha watoto katika shule hiyo ambayo januari 2023 itapokea watoto wa kuanza kidato cha kwanza.
Nae Diwani wa kata ya Makurunge, Hamisi Mohamed, amesema wananchi wa kata hiyo wamefurahishwa sana na ujenzi wa shule ya sekondaari katika kata hiyo na wapo tayari kutoa ushirikiaano wao pindi watakapohitajika kufanya hivyo.
Amesema ili kuthibisha kuwa wananchi hao wamefurahishwa na ujenzi huo, wamejitokeza kwa wingi katika uzinduzi wa ujenzi huo katika haatua ya awali ya kuchimba msingi wa madarasa.
Kwa upande wake Mtendaji kata Makurunge Chumi Joel amesema amefanikiwa kuunganisha nguvu za wananchi wa kata yote kupitia wenyeviti wa vitongoji ndani ya kata hiyo ambapo kila mwenyekiti wa kitongoji amfika na wananchi wake na kushiriki kazi kikamilifu.
Aidha, amewataka wananchi wa kata hiyo kuwa tayari kujitolea katika kazi za maendeleo ili kufanikisha malengo yao ndani ya kata.
Nao wazazi wa kata ya Makurunge wamemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwa kuwatengea fedha hizo za ujenzi wa shule ya sekondari ili watoto wao sasa wapate kusoma shule iliyo karibu nao.
Wahandisi kutoka idara ya ujenzi Halmashauri ya Bagamoyo wakihakiki vipimo vilivyopo kwenye michoro katika zoezi la uchimbaji msingi wa shule mpya ya sekondari inayojengwa katika Kitongoji cha Geza ulole Kata ya Makurunge.
Wananchi wa kata ya Makurunge Halmashauri ya Bagamoyo, wakishiriki zoezi la uchimbaji msingi katika ujenzi wa shule mpya ya sekondari inayojengwa katika Kitongoji cha Geza ulole kata ya Makurunge.
Wananchi wa kata ya Makurunge Halmashauri ya Bagamoyo, wakishiriki zoezi la uchimbaji msingi katika ujenzi wa shule mpya ya sekondari inayojengwa katika Kitongoji cha Geza ulole kata ya Makurunge.
Mtendaji kata Makurunge, Chumi Joel akishirikiana na Wananchi wa kata hiyo iliyopo Halmashauri ya Bagamoyo, katika zoezi la uchimbaji msingi wa ujenzi wa shule mpya ya sekondari inayojengwa katika Kitongoji cha Geza ulole kata ya Makurunge.
Mtendaji kata Makurunge, Chumi Joel akishirikiana na Wananchi wa kata hiyo iliyopo Halmashauri ya Bagamoyo, katika zoezi la uchimbaji msingi wa ujenzi wa shule mpya ya sekondari inayojengwa katika Kitongoji cha Geza ulole kata ya Makurunge.
Wananchi wa kata ya Makurunge Halmashauri ya Bagamoyo, wakiwa na nyuso za furaha wakati wa wakishiriki zoezi la uchimbaji msingi katika ujenzi wa shule mpya ya sekondari inayojengwa katika Kitongoji cha Geza ulole kata ya Makurunge.
No comments:
Post a Comment