Posts

CUBA KUONGEZA NGUVU ZAIDI ITALIA

Image
Na Albert Kawogo. Cuba inatafakari namna ya kuongeza kikosi kingine cha madaktari ili kuongezea nguvu kasi ya huduma kwa wagonjwa wa corona nchini Italia. Tayari kikosi cha kwanza Cha madaktari 100 na vifaa tiba kilikwisha ingia nchini humo mwanzoni mwa juma hili huu ukiwa ni uamuzi uliofikiwa na serikali ya Cuba kusaidia jitihada za nchi ya Italia kuokoa uhai wa raia wake. Zaidi ya waitaliano 80,000 wameambukiwa virusi vya corona hii ikielezwa kuwa ni idadi kubwa kufikiwa na nchi moja barani Ulaya tangu ugonjwa huo ulipoingia Italia miezi miwili iliyopita. Wizara ya afya ya Cuba imeonyesha nia ya kuongeza madaktari zaidi ili kuunganisha juhudi za serikali ya Italia kupambana na ugonjwa huo ambao wastani wa watu 600 hufariki kila siku nchini humo. Pamoja na serikali ya Cuba kuishi katika kisima cha vikwazo vya kiuchumi kwa miaka 56 sasa vinavyotokana na shinikizo la Marekani bado serikali hiyo imekuwa ni ya pili kuonyesha nia ya kuisaidia Italia baada ya...

RAIS MAGUFULI AMTEUA BRIGEDIA JENERALI MBUNGO KUWA MKURUGENZI WA TAKUKURU

Image
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Kaimu Mkurugenzi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana Rushwa (TAKUKURU) Brig. Jenerali John Mbungo kuwa Mkurugenzi wa taasisi hiyo kwa kazi nzuri aliyoifanya ikiwemo ya kurejesha bilioni 8.8 walizodhulumiwa wananchi. Rais amefanya uteuzi huo leo, Machi 26, 2020 katika hafla ya kupokea ripoti kutoka Ofisi ya Mkaguzi Mkuu wa Serikali CAG na ripoti ya TAKUKURU katika Ikulu ya Chamwino Jijini Dodoma.

HADI SASA TUMEWEZA KUDHIBITI MAAMBUKIZI YA NDANI KWA NDANI YA CORONA-WAZIRI UMMY

Image
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazeena Watoto, Ummy Mwalimu, akiwa na Waziri wa Afya wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mhe. Hamad Rashid na Naibu Katibu Mkuu wake wakati akiongea na Waandishi wa Habari juu ya mwenendo wa ugonjwa wa Corona (COVID-19) Jijini Dodoma. ................................... Na WAMJW-DOM. Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazeena Watoto, Ummy Mwalimu, amebainisha kuwa, hadi sasa Tanzania imeweza kudhibiti maambukizi ya ndani kwa ndani ya ugonjwa (COVID-19) na kuwasisitiza wananchi kuendelea kuchukua tahadhari zote za kujikinga. Amesema, wasafiri 245 walioingia Tanzania Bara na Zanzibar tangu Machi 23, mwaka huu, wametengwa kwenye hoteli na maeneo yaliyoandaliwa na Serikali kwa gharama zao. Waziri Ummy ametoa kauli hiyo leo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma, kuhusu mwenendo wa ugonjwa wa Corona nchini. Amesema hadi sasa hakuna maambukizi ya ndani (Local transmission) na wag...