Na
Albert Kawogo.
Cuba
inatafakari namna ya kuongeza kikosi kingine cha madaktari ili kuongezea nguvu
kasi ya huduma kwa wagonjwa wa corona nchini Italia.
Tayari
kikosi cha kwanza Cha madaktari 100 na vifaa tiba kilikwisha ingia nchini humo
mwanzoni mwa juma hili huu ukiwa ni uamuzi uliofikiwa na serikali ya Cuba
kusaidia jitihada za nchi ya Italia kuokoa uhai wa raia wake.
Zaidi
ya waitaliano 80,000 wameambukiwa virusi vya corona hii ikielezwa kuwa ni idadi
kubwa kufikiwa na nchi moja barani Ulaya tangu ugonjwa huo ulipoingia Italia
miezi miwili iliyopita.
Wizara
ya afya ya Cuba imeonyesha nia ya kuongeza madaktari zaidi ili kuunganisha
juhudi za serikali ya Italia kupambana na ugonjwa huo ambao wastani wa watu 600
hufariki kila siku nchini humo.
Pamoja
na serikali ya Cuba kuishi katika kisima cha vikwazo vya kiuchumi kwa miaka 56
sasa vinavyotokana na shinikizo la Marekani bado serikali hiyo imekuwa ni ya
pili kuonyesha nia ya kuisaidia Italia baada ya awali China pia kupeleka
madaktari wake nchini humo.
Umoja
wa Ulaya EU umekuwa lawamani kwa kushindwa kuweka mikakati ya kuisaidia Italia
iliyoathirika zaidi na corona ambapo siku kadhaa zilizopita waitaliano wamekata
tamaa na umoja huo hatua iliyowafanya baadhi yao kushusha bendera ya Umoja huo
kwenye miji mbalimbali na kupandisha bendera za Cuba na China kama mbadala
wake.
Waziri
Mkuu wa Italia Giusepe Conte ameonya kuwa hali huenda ikawa mbaya zaidi iwapo
waitaliano watapuuzia amri ya kukaa ndani.
"Virusi
havitembei bali vinatembezwa na watu, tusipotembea navyo havitatembea na baadae
vitakufa vyenyewe" Alisema Conte.
Conte
ametoa wito kwa EU kuona namna ya kusaidia nchi zote wanachama zilizoathirika
sana ili kupunguza kasi ya kuenea kwa maambukizi ya ugonjwa huo barani Ulaya.
No comments:
Post a Comment