Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,
Wazeena Watoto, Ummy Mwalimu, akiwa na Waziri wa Afya wa Serikali ya Mapinduzi
ya Zanzibar Mhe. Hamad Rashid na Naibu Katibu Mkuu wake wakati akiongea na
Waandishi wa Habari juu ya mwenendo wa ugonjwa wa Corona (COVID-19) Jijini
Dodoma.
...................................
Na WAMJW-DOM.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,
Jinsia, Wazeena Watoto, Ummy Mwalimu, amebainisha kuwa, hadi sasa Tanzania
imeweza kudhibiti maambukizi ya ndani kwa ndani ya ugonjwa (COVID-19) na
kuwasisitiza wananchi kuendelea kuchukua tahadhari zote za kujikinga.
Amesema, wasafiri 245 walioingia
Tanzania Bara na Zanzibar tangu Machi 23, mwaka huu, wametengwa kwenye hoteli
na maeneo yaliyoandaliwa na Serikali kwa gharama zao.
Waziri Ummy ametoa kauli hiyo leo
alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma, kuhusu mwenendo wa
ugonjwa wa Corona nchini.
Amesema hadi sasa hakuna maambukizi
ya ndani (Local transmission) na wagonjwa 13 waliothibitika kuwa na virusi vya
ugonjwa huo wanaendelea vizuri.
“Hatua mbalimbali zimechukuliwa kwa
lengo lakutimiza dhamira nzuri ya serikali ya kupunguza hatari ya kusambaa kwa
haraka maradhi haya nchini, tunashukuru Mungu bado hatuna ‘Local
transmission,”amesema.
Aidha, amesema mgonjwa wa kwanza wa
Arusha, amepona Corona na taratibu za kumruhusu kurudi nyumbani zinaendelea.
“Mgonjwa wetu amepona COVID19 na
amepimwa mara tatu hana, tumeanza utaratibu wa kumrudisha nyumbani, kazi ambayo
nimemuelekeza Katibu Mkuu aifanye sasa hivi suala la kutoa elimu ili kuondoa
unyanyapaa, kulaumiana na kunyoshewa vidole Isabela,” amesema.
Kadhalika, amesema wasafiri hao 245
wamewekwa karantini kwa siku 14 kwenye maeneo maalum ikiwa ni utekelezaji wa
agizo la Rais, Dkt.John Pombe Magufuli.
“Tangu agizo la Rais wasafiri 111 kwa
Tanzania barana 134 kwa Zanzibar wametengwa kwenye hayo maeneo, na tunasisitiza
mikoa yote nchini kuendelea na zoezi la kubainisha sehemu zitakazo tumika
kuweka wasafiri bila kuleta usumbufu usio wa lazima,”amesema.
Pamoja na hayo, Waziri huyo amesema
Wizara ya Afya kwa kushirikiana na Wizara ya Afya ya Zanzibar imeendelea
kufanya ukaguzi kwa kupima joto lamwili kwa wasafiri wote wanaoingia nchini.
“Kuanzia Januari mosi mwaka huu hadi
sasa wasafiri 1,890,532 wamefanyiwa ukaguzi wa kupimwa joto kwenye vituo 27 vya
mipakani ikiwemo viwanja vya ndege na bandarini na kwa saa 24 zilizopita jumla
yawasafiri 3,471 wamefanyiwa ‘screening’,”amesema.
Amefafanua kuwa watu 273 wamepimwa
sampuli za kupima virusi vya Corona katika Maabara Kuu ya Taifa ya Afya ya
Jamii hadi Machi 26,2020.
“Kati ya sampuli hizo zilizopimwa 260
hazikuonesha uwepo wa virusi hivyo na sampuli 13 zilithibitika kuwa na virusi,
wagonjwa hawa ni kutoka Mkoa wa Arusha (2), Dar es salaam(8), Zanzibar (2) na
Kagera (1),”amesema.
Katika hatua nyingine, Waziri huyo
ameshukuru msaada wa vifaa mbali mbali ikiwemo vya kupima virusi haraka (Rapid
test kits) kutoka kwa Taasisi zilizopo Jamhuri ya watu wa China za Jack Ma na
Alibaba na vitasambazwa kwenye hospitali zilizotengwa maalum kwa ajili ya
kuhudumia wagonjwa hao.
Waziri Ummy
amesema maabara iliyopo haijazidiwa na utaratibu mzuri umeandaliwa wa upimaji
wa sampuli kutoka mikoani.
Aidha, amesema serikali inatarajia
kuongeza maabara sita na Zanzibar moja.
“Tumeona pia kuna haja ya kuongeza
maabara, tayari maabara ya Chuo Kikuu Sokoine (Sua) inaweza kupima sampuli, pia
maabara za NIMR Mbeya, Tanga, Mwanza na Arusha ile maabara ya St.Nelson
Mandela, hili tumeliona lakini tumeona kuna haja ya kuwa na ‘rapid test’, tupo
vizuri hatujazidiwa na sampuli zinafika kwa wakati kwenye maabara
yetu,”amesema.
Waziri huyo amesema vipimo vya kupima
virusi kwa haraka vitawekwa kwenye Hospitali za Mikoa, Kanda na kwenye mipaka.
“Jumuia ya ya Afrika Mashariki pia
jana tumepata msaada wa maabara zinazotembea, na tuta pata mbili kwa Tanzania
ambazo zitapelekwa Arusha na Zanzibar,”amesema.
Naye, Waziri wa Afya Zanzibar, Hamad
RashidMohammed, amewataka Watanzania kujikinga na ugonjwa huo huku akisisitiza
kuwa Serikali haina nia ya kumuweka mtu kambini kumtesa.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,
Wazeena Watoto, Ummy Mwalimu, akieleza jambo, wakati akiongea na Waandishi wa
Habari juu ya mwenendo wa ugonjwa wa Corona (COVID-19) Jijini Dodoma.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,
Jinsia, Wazeena Watoto, Dkt. Faustine Ndugulile akiwa na Katibu Mkuu Wizara ya
Afya Dkt. Zainab Chaula wakifuatilia neno kutoka kwa Waziri wa Afya Mhe. Ummy
Mwalimu (hayupo kwenye picha, wakati akiongea na Waandishi wa Habari juu
ya mwenendo wa ugonjwa wa Corona (COVID-19) Jijini Dodoma.
No comments:
Post a Comment