CUBA KUONGEZA NGUVU ZAIDI ITALIA
Na Albert Kawogo. Cuba inatafakari namna ya kuongeza kikosi kingine cha madaktari ili kuongezea nguvu kasi ya huduma kwa wagonjwa wa corona nchini Italia. Tayari kikosi cha kwanza Cha madaktari 100 na vifaa tiba kilikwisha ingia nchini humo mwanzoni mwa juma hili huu ukiwa ni uamuzi uliofikiwa na serikali ya Cuba kusaidia jitihada za nchi ya Italia kuokoa uhai wa raia wake. Zaidi ya waitaliano 80,000 wameambukiwa virusi vya corona hii ikielezwa kuwa ni idadi kubwa kufikiwa na nchi moja barani Ulaya tangu ugonjwa huo ulipoingia Italia miezi miwili iliyopita. Wizara ya afya ya Cuba imeonyesha nia ya kuongeza madaktari zaidi ili kuunganisha juhudi za serikali ya Italia kupambana na ugonjwa huo ambao wastani wa watu 600 hufariki kila siku nchini humo. Pamoja na serikali ya Cuba kuishi katika kisima cha vikwazo vya kiuchumi kwa miaka 56 sasa vinavyotokana na shinikizo la Marekani bado serikali hiyo imekuwa ni ya pili kuonyesha nia ya kuisaidia Italia baada ya...