TGNP kufanya mapitio ya sera na ilani za vyama vya siasa nchini
TGNP Mtandao imepanga kufanya mapitio ya sera na ilani za vyama vya siasa kwa mrengo wa kijinsia na kushauri kufanya marekebisho mapema kabla ya uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020. Viongozi mbalimbali wa chama cha ACT Wazalendo wakiwa katika picha ya pamoja na wageni wao kutoka TGNP Mtandao, wakionesha Ilani ya uchaguzi ya mwaka 2019 iliyotengenezwa na TGNP Mtandao kwa kushirikiana na wadau wengine wa haki za wanawake. Akizungumza wakati wa ziara ya kukabidhi ilani ya madai ya wanawake katika uchaguzi wa serikali za Mitaa wa mwaka 2019 na uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020 kwa chama cha ACT wazalendo, Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP Mtandao Lilian Liundi, alisema kwamba baada ya kutembelea vyama kadhaa vya siasa nchini na kusikiliza jinsi wanavyotekeleza masuala ya kijinsia, ameona kuwa kuna haja ya TGNP na Mashirika mengine yanayotetea haki za wanawake na Usawa wa Jinsia, kufanya uchambuzi au mapitio ya sera na ilani za vyama kwa mrengo wa kijinsia na kuangalia mapengo ili kushauri...