Posts

WAZIRI KALEMANI AWASHA UMEME KIJIJI CHA MWAKITOLYO SHINYANGA.

Image
Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani (aliyeinua mkono), akifurahi na viongozi mbalimbali wa Serikali na Chama Cha Mapinduzi (CCM), baada ya kukata utepe kuashiria uwashaji rasmi wa umeme katika Kijiji cha Mwakitolyo, Shinyanga Vijijini, Juni 29, 2019.  Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani akizungumza na wananchi wa Kata ya Mwakitolyo, Shinyanga Vijijini, muda mfupi kabla ya kuwasha rasmi umeme katika eneo hilo, Juni 29, 2019 akiwa katika ziara ya kazi. ....................................... Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani ametimiza ahadi yake aliyoitoa mwanzoni mwa mwezi huu (Juni) 2019 kwa wananchi wa Kijiji cha Mwakitolyo, Shinyanga Vijijini, kuwa umeme utawashwa katika eneo lao kabla ya Julai, 2019. Dkt. Kalemani alitimiza ahadi hiyo jana, Juni 29, 2019 akiwa katika ziara ya kazi mkoani Shinyanga, ambapo aliwasha rasmi umeme katika jengo la Ofisi ya Serikali, Kitongoji cha Mwakitolyo Namba Tano. Akizungumza na wana...