MGOMBEA UDIWANI LINDI (CUF) ALALAMIKIA WASIMAMIZI WA UCHAGUZI.
Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) BI Rukia Mbasha akimkabidhi ilani ya chama hicho Diwani mteule wa kata ya Mvuleni Mnuli Saidi Khatibu Baada ya kutangazwa na Msimamizi kuwa Amepita kuwa diwani wa kata hiyo Bila kupingwa Diwani Mteule wa kata ya Mvuleni Mnuli Khatibu (CCM) akionyesha ilani ya Chama hicho baada ya kukabidhiwa ................................. Na Hadija Hassan, Lindi. MGOMBEA Udiwani Kata ya Mvuleni, Halmashauri ya Lindi, Mkoani hapa, Chuma Abdurahamani Saidi (CUF) amesikitishwa na maamuzi yaliyofanywa na wasimamizi wa uchaguzi mdogo Wilayani Hapa kumpitisha mpinzani wake, Mnuli Said Khatibu {CCM} Kuwa Diwani wa kata hiyo kwa madai ya kushindwa kujibu pingamizi zake. Chuma ametoa masikitisho hayo wakati alipokuwa akizungumza na Mwandishi wa Habari hiziz, kuhusu kutupiliwa mbali kwa pingamizi lenye vipengele vinne alizokuwa amemuwekea mpinzani wake Mnuli Said Khatibu wa Chama Cha Mapinduzi {CCM}. ...