CHAHUA WAKUMBUKA HOFU YA RIDHIWANI KIKWETE KUHUSU MAJI
Wakazi wa kitongoji cha Chahua, kata ya Bwilingu Halmashauri ya Chalinze wilayani Bagamoyo wakiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi wao mara baada ya zoezi la usafi la kila mwisho wa mwezi ambapo wakazi hao walijumuika kwenye Zahanati yao kwaajili zoezi hilo, Picha na Omary Mngindo. .............................................................. Na Omary Mngindo, Chahua MWENYEKITI wa Kitongoji cha Chahua, Kata ya Bwilingu Halmashauri ya Chalinze mkoani Pwani Rashid Maisha, amekumbuka hofu iliyooneshwa na Mbunge wao Ridhiwani Kikwete, aliyeionesha wakati ikitolewa ahadi ya upatikanaji wa maji jimboni humo, ifikapo Des 31 mwaka huu. Maisha ametoa kauli hiyo mwishoni mwa wiki, akizungumza na mwandishi wa habari hizi muda mfupi mara baada ya kumalizika kwa zoezi la usafi wa mwishoni mwa mwezi, ambapo wakazi hao walijumuika kwenye jengo la Zahanati kwa ajili ya zoezi hilo. Alisema kwamba, kwenye mkutano uliofanyika hivi karibuni mbele ya Makamu w...