VICTOR MASANGU, PWANI.
JESHI la
Polisi Mkoa wa Pwani linawasaka watu sita wanaodhaniwa kuwa ni
majambazi baada ya kuvamia katika kiwanda cha kutengenezea vifungashio
kilichopo maeneo ya Picha ya ndege Wilayani Kibaha nakufanikiwa kuiba kiasi cha
shilingi milino 3, simu nne za mkononi, pamoja na kompyuta mpakato mbili.
Akizungumza
na waandishi wa habari Ofisni kwake Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Kamisshna
Msaidizi wa Polisi (ACP) Wankyo Nyigesa, amesema kwamba tukio hilo limetokea
usiku wa kumakia leo majira ya tisa
usiku ambapo pia waliwashambulia wamiliki wa kiwanda hicho wakiwa na silaha
mbali mbali za jadi ikiwemo marunga, mapanga, na nondo na kukimbilia
pasipojulikana na kwamba walinzi wa kiwanda hicho wanashikiliwa.
Katika
hatua nyingine Kamanda Wankyo amebainisha kuwa Polisi mkoani humo imewakamata
watu nane akiwemo daktari wa idara ya mifugo kwa tuhuma za
kujihusisha na wizi wa mifugo aina ya mbuzi na kondoo pamoja na kuuza
nyama ya ng’ombe kilo 405 isiyokaguliwa katika eneo la halmashauri ya Chalinze
Wilayani Bagamoyo Mkoa wa Pwani ambapo watuhumiwa wote wamefikishwa mahakamani.
No comments:
Post a Comment