Na
Shushu Joel
WANANCHI
wa Mbagala jijini Dar es Salaam wamevutiwa na kitendo Cha Mamlaka ya Mapato
Tanzania (TRA) kuwapelekea huduma ya utoaji Namba ya Utambulisho wa Mlipakodi
(TIN) zoezi ambalo linaloendeshwa katika mkoa huo.
Wakizungumza
mara baada ya kusajiliwa na kuwa walipakodi wafanyabiashara wa maeneo hayo
wamekoshwa na huduma ya kufuatwa mahali walipo.
Monira
Said ni mmoja wa wateja waliopatiwa huduma za TIN kwa mara ya kwanza alisema kuwa
huduma wanazozitoa watu wa TRA ni zenye kiwango cha kipekee.
"Nimefurahia
sana kukabidhiwa TIN yangu kwa mara ya kwanza tena bure huku nilikuwa nikijua
labda huduma hii ni ya malipo kumbe hapana" Alisema.
Aliongeza
kuwa kwa wale ambao hawajachangamkia nafasi hii ni bora wakajitokeza mapema
hili waweze kupata huduma za TRA kwani mafanikio makubwa watayaona mara baada
ya kuwa katika mfumo wa TRA.
Aidha,
alitoa ushauri kwa maofisa wa TRA kuwa mbagala kwa sasa ni moja ya sehemu
zinazokuwa kibiashara na moja ya maeneo yenye biashara kubwa hapa jijini Dar es
Salaam kama kariakoo.
Naye
Haji Khareed ni mwenyekiti wa wafanyabiashara wa nguo katika soko la mbagala
alisema kuwa tangu vijana wengi walikuwa wakiwasubili Kwa hamu kubwa watu wa
mamlaka ya mapato (TRA) ili wawaelimishe juu ya umuhimu wa kulipa kodi.
Aliongeza
kuwa kufuatwa kwa wateja kwenye maeneo yao ya kazi kumewafanya kujiona ni watu
wenye thamani sana katika nchi hii.
"Ukilipa
kodi unasaidia nchi kutekeleza miradi mikubwa ya kimaendeleo hivyo kila mmoja
wetu awajibike katika kulipa kodi na faida lazima aione "Alisema
mwenyekiti Khareed.
Naye
Afisa mwandamizi wa elimu kwa mlipa kodi Catherine Mwakilagala amewashukuru
wafanyabiashara wa mbagala kwa kujitokeza kwa wingi kwa ajili ya kupata huduma
toka TRA.
Hivyo
amewataka kuendelea kujitokeza pindi wanaposikia watendaji wa mamlaka ya mapato
Tanzania (TRA) wamekuja waweze kujitokeza kwa wingi ili kupatiwa huduma. Aidha
amewapongeza wakazi wa mbagala kwa kumiminika kujitokeza kupata huduma za
elimu.
No comments:
Post a Comment