Kamanda wa Polisi mkoa wa morogoro, Kamishna
Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Wilbroad Mutafungwa, akiwaonyesha
wanahabari (hawapo pichani ) panga na msumeno alivyokutwa navyo, bwana Benson
Benard (31) aliekutwa Uchi wa Mnyama yeye na Mtoto wake katikati ya Maporomoko
ya Maji eneo la Mlimani, Nguzo Camp.
............................................
Na farida saidy morogoro
Jeshi La Polisi Mkoa wa Morogoro linamshikilia
Benson Benard (31) aliyekutwa Uchi wa Mnyama yeye na Mtoto wake katikati ya
Maporomoko ya Maji eneo la Mlimani Nguzo Camp ndani ya manispaa hiyo.
Mtu huyo alipoamuliwa kuondoka eneo hilo hatarishi akajirusha na kujizamisha kwenye Maji
yaliyokuwa yakitiririka kwa kasi kabla ya kushikiliwa na Polisi.
Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi mkoa
wa Morogoro, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Wilbroad Mutafungwa Askari
wake walipokea taarifa toka kwa raia mwema juu ya uwepo wa tukio hilo na baada ya
kufika eneo la tukio ambapo ni eneo la chanzo cha maji wakamkuta
mtuhumiwa akiwa na Mtoto wake, na katika hali ya kushangaza wote walikua uchi
wa mnyama.
Aidha katika
Eneo hilo la Tukio Askari Polisi walikuta Panga na Msumeno ambapo pia kunadaiwa
kumefanyika uharibifu wa mabomba ya maji, na sasa mtuhumiwa anashikiliwa na
Polisi kwa mahojiano.
Hata hivyo Mtoto
amekabidhiwa kwa mama yake mzazi Mary Shao mkazi wa Kihonda, ambae nae anasema
mumewe alianza kubadilika kwa kuongea mambo yasiyo eleweka na siku hiyo ya
tukio aliaga anaenda kuogelea.
No comments:
Post a Comment