Serikali imesema hadi sasa imefanikiwa kusajili laini milioni 19.681.086 kwa alama za vidole ambayo ni sawa na asilimia 42 zinazomilikiwa na watu mil 7.6 ikiwa zimebaki siku 18 ya zoezi hilo lifikie mwisho.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Mhandisi James Kilaba alipokua wakielezea hali ya usajili wa laini za simu za mkononi kwa njia ya alama za vidole kuanzia Mei Mosi mwaka huu hadi Desemba 13 mwaka huu.
Amesema kuwa wananchi wanatakiwa kufuata taratibu za kuweza kupata vitambulisho vya taifa ili kuweza kusajili laini za simu kwa kutumia alama za vidole.
Kilaba amesema kuwa watu waache kufuata taarifa ambazo hawana uhakika nazo kwani kuamini taarifa zisizo sahihi ni kutaka kukwamisha zoezi hilo
Amesema pia idadi ya laini ambazo wamiliki wana namba za utambulisho za NIDA (NIN) lakini hawajasajili kwa njia ya alama za vidole ni milioni 5.599.610 ambazo zinamilikiwa na takribani watu milioni tatu.
“Laini za simu zisizosajiliwa kwa alama za vidole ni milioni 21.782 .906 ambazo zinamilikiwa na takribani watu milioni 10.5,” amesema.
Nae Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), Dkt. Arnold Kihaule amesisitiza kasi ya uandikishaji NIDA kwani kuna manufaa mengi huku akisema idadi ya watu wasiopata vitambulisho au namba za NIDA na kwamba hawafanyi lolote zaidi ya milioni tatu.
Dkt.Kihaule amesema kuwa na wanamfumo wa kuangalia na kuweza kupata namba ya kitambulisho cha taifa kwa kuweka jina la kwanza na kuweka nyota jina la ukoo,nyota, Tarehe yakuzaliwa mwezi na mwaka kwa kuunganisha,nyota jina la Mama,nyota jina la baba na kutuma kwa namba 15096.
Katika mfano IMA*ALI*25071985*AMINA*SAID na kutuma kwenda namba 15096 hivyo kila mtu alifanya usajili kwa kupiga picha hatua za mwisho.TV
No comments:
Post a Comment