Mganga Mkuu Ruvuma Dr.Jairy Khanga
|
Joyce
Joliga,Songea
Watoto
1101 kati ya 4612 walipata matibabu ya utapiamlo mkali katika vituo
vya kutolea huduma za afya ambapo lengo ni kuwafikia watoto
wanaosadikika kua na utapiamlo Mkali kutokana na takwimu za Survey.
Akizungumza na Mwananchi Mganga
Mkuu mkoa wa Ruvuma Dkt.Jairy Khanga alisema watoto hao
walipatiwa matibabu katika
kipindi cha mwezi July 2018 hadi June 2019, ambapo takwimu
za National nutrition survey 2018 zinaonesha mkoa wa Ruvuma bado ni miongoni
mwa mikoa yenye hali duni ya lishe kwa watoto chini ya miaka mitano ikiwa
udumavu ni 41% kitaifa ikiwa ni 31.8%, Ukondefu kwa watoto ni 3% kitaifa ikiwa
ni 4% na uzito pungufu ikiwa ni 16.5% kitaifa ikiwa ni 14.6%.
Alisema, Utapiamlo
huathiri afya, uzalishaji mali na maendeleo katika jamii. Athari hizo
hujitokeza kwa njia mbali mbali kama Kupungua kwa uwezo wa akili hivyo watoto
kupata ugumu wa kufundishika na kuelewa Kuchelewa katika hatua za
ukuaji wa mtoto kimwili na kiakili.
Anazitaja athari nyingine
ni Kuongezeka kwa magonjwa na vifo vya watoto
Ikiwa ni pamoja
na Kuongezeka kwa magonjwa na vifo kwa wanawake wajawazito
na Kupungua kwa kinga ya mwili
na Kuongezeka kwa walemavu, mfano mgono wazi na vichwa vikubwa na
Kupungua kwa uwezo wa kufanya kazi na uzalishaji mali.
Kwa upande wake Ofisa Lishe
Mkoa Eugenia Kombeo alisema, , tayari mikakati mbalimbali imewekwa
ili kuboresha hali za lishe za watoto wadogo ikiwa ni pamoja na Elimu ya lishe
kutolewa ipasavyo katika vituo vya kutolea huduma za afya na katika Jamii
kupitia wahudum wa afya ngazi ya vijiji kwa wajawazito na wamama wanaonyonyesha
,kuanzia July 2018 hadi june 2019 wamama na walezi 60865wenye watoto wenye miez 0-23 walipatiwa
elimu ya usahihi wa ulishaji wa watoto wachanga na wadogo.
Naye Aureria Mhagama mkazi wa Mshangano
alisema tatizo la Lishe duni limechangiwa na baadhi ya wakinamama kutohudhuria
kliniki hivyo kukosa elimu sahihi hali ambayo imesababisha watoto wengi kudumaa
na wengine kupoteza maisha.
No comments:
Post a Comment