Na
Shushu Joel.
WANANCHI wa Buza jijini Dar es Salaam wamejitokeza kwa wingi kwenye banda la utoaji wa huduma na Elimu kwa mlipa kodi.
WANANCHI wa Buza jijini Dar es Salaam wamejitokeza kwa wingi kwenye banda la utoaji wa huduma na Elimu kwa mlipa kodi.
Wakizungumza
kwa wakati tofauti mara baada ya kuhudumiwa na kukabidhiwa kwa vyeti vyenye
Namba ya Utambulisho wa Mlipakodiza, wameipongeza mamlaka hiyo kwa kuwapelekea
huduma milangoni mwao.
Gift
Bosco (47)ni mkazi wa buza ninaipongeza mamlaka ya mapato Tanzania kwa utoaji
wake wa elimu kwa kutufuata wakazi wa buza.
"Nimefanikiwa
kupata TIN ninaamini huu ni mwanzo wa kuwa miongoni mwa walipa kodi
wazuri"
Aliongeza
kuwa wananchi wengi hawana uelewa juu ya umuhimu wa kulipa kodi hivyo wawe
wanaangalia vipindi vya TRA kwenye TV kwani vinaelimisha sana kuhusu umuhimu wa
kulipa kodi.
Aidha
amewataka mamlaka ya mapato kuendelea kuwatembelea na kuwaelimisha kwani uelewa
unaongezeka siku hadi siku.
Naye
Muhammad Ally ni mmoja wa wakazi wa Buza na ni mfanyabiashara wa duka amesema
kuwa miaka ya nyuma ukiwaona watu wa mamlaka ya mapato Tanzania wanakuja basi
unaenda kufunga duka na wewe kwenda kujificha lakini kutokana na elimu pana inayotolewa
na mamlaka hiyo wengi wamekuwa waelewa juu ya ulipaji wa kodi.
Aidha,
Ally amesifu utendaji wa kazi wa TRA kwa kuwafikia wateja wake tena majumbani
kabisa.
Kwa
upande wake Meneja wa Elimu kwa mlipa kodi Diana Masalla kutoka TRA alisema
kuwa zoezi la utoaji wa elimu linaendelea kila mahali kwa lengo la kuwaelimisha
wananchi zaidi.
Hivyo
amewapongeza wananchi wa buza kwa namna walivyojitokeza kusikiliza na
kuelimishwa umuhumi wa kuwa na TIN na kulipia kodi ya majengo.
Aidha
Masalla aliongeza kuwa TRA itaendelea kutoa elimu kwa kila mwananchi ili aweze
kunufaika na biashara yake anayoifanya kwani wafanyabiashara wengi wamekuwa
wakifeli kutokana na ukosaji wa elimu.
"TRA
imetambua thamani yenu na ndio maana tumeamua kuwafuata karibu na biashara zenu
ili msifunge na kutufuata mbali sasa tunakufuata mlangoni kwako ili
tukuhudumie"
No comments:
Post a Comment