Joyce Joliga,Songea
Bado kuna changamoto kubwa ya wanafunzi
kupatiwa chakula wakati wa masomo hali ambayo imechangia wanafunzi
wengi kukatisha masomo, kufeli mithiani yao na ongezeko la utoro .
Kufatia hali hiyo Wadau wa
Elimu mkoani Ruvuma
wameitaka Wizara ya elimu kuwabana Wazazi
na walezi wa watoto
wanaosoma madarasa ya awali na shule za
msingi ili waweze kuchangia gharama za chakula cha watoto wao wakati
wakiwa shuleni hivyo kuwasaidia wafanye vizuri kwenye masomo yao na
kuondokana na madhara ya kiafya ikiwemo vidonda vya tumbo
, utoro, wizi na unyanyapaa.
kwa mujibu wa
ripoti ya Makadirio ya watu (National Population
Projections) iliyotolewa na Bodi ya Taifa yaTakwimu NBS feb 2018
Makadirio ya idadi ya watoto wenye umri wa
kati ya miaka 5 mpaka 8 mwaka 2018 kulikuwa
na watoto 5, 888,072 na 2019 ilikadiriwa kuwa Tanzania
itakuwa na watoto 6,184,084
Aidan Hyella ni
mdau wa elimu na Mzazi anatoa ushauri
kwa Wazazi kushirikiana na uongozi
wa shule waweke mikakati ya pamoja ili
kuweza kuhakikisha watoto wanapata chakula wakiwa shuleni hivyo
kuondokana na tatizo la kufeli mithiani na kuzimia kutokana na njaa
Anasema, mkoa wa Ruvuma
umebarikiwa kuwa na chakula kingi lakini bado shule nyingi
hazina huduma ya chakula shuleni hali ambayo inamkosesha mtoto
haki ya msingi yakupata milo mitatu na hivyo kudhoofisha akili
na mwili”
“Tubadilike wazazi hivi tunajisikia
Amani watoto wetu wanashinda na njaa sisi tunakula , nafikiri wakati umefika
sasa wa kuwasaidia hawa watoto kupata chakula mashuleni kwani ile
Shea yake ambayo angekula akiwa nyumbani ndio atakayokula akiwa shuleni,
tuache ubinafsi tuchangie chakula cha watoto wetu,”anasema Aidan
Samimu Ngonyani ni mwanafunzi wa
Darasa la pili shule yamsingi Luhila anasema
kukosekana chakula shuleni ni mateso kwa wanafunzi kwani
wanaondoka nyumbani bila kimywa chai hivyo Wapo wanaotembea umbali mrefu
kwenda shule na wakati mwingine uamua kuishia njiani na kuomba omba
pesa kwa watu na ukifika muda wa kurudi nyumbani nae anarudi.
“Natamani
tupewe chakula shuleni kama darasa la Saba na la nne wao
wanakula chakula cha shule Sisi tunashinda na njaa na
walimu hawatuonei huruma,”anasema
Naye Jumanne
Msabaha mwalimu mkuu wa shule ya msingi
Skill path iliyopo Manispaa ya Songea amesema,
tatizo la watoto kutokula shuleni linachangia kufeli kwa wanafunzi
kwani wazazi wengi hawataki kuchangia gharamaya chakula cha Watoto
wao hali ambayo inawafanya watoto wengi kukosa
haki ya kupata chakula wakati wa masomo ingawa
wapo baadhi ya wazazi ambao ujitoa na kuchangia gharama
hizo.
Ametoa mfano kuwa shule hiyo
ina wanafunzi 885 ni wanafunzi 194 tu ndio
wanaopata chakula shuleni ambapo kati
yao wanafunzi wenye umri wa mika 3-8 ambao
wanasoma chekechea na wali wapo 240 ambapo
wanatakiwa kupata uji wa lishe , chai na chakula cha
mchana lakini hawapati kutokana na wazazi wao kutochangia gharama.
“Tumeshakaa vikao na
wazazi si chini ya vitano vya kuwaelekeza umuhimu wa
watoto kupata chakula shulenilakini bado kuna changamoto
wapo wazazi wanakubali kulipa na wapo wanaopinga kwa madai kuwa wanawapa watoto
wao pesa za matumizi , hivyo kusababisha watoto kushinda na njaa , watoto
wanadondoka kutokana na njaa utakuta mtoto ametoka nyumbani saa 11 alfajiri na
hajaandaliwa chochote hivyo ikifika saa mbili anashindwa kuendelea
na masomo kutokana na njaa kali,”alisema Msabaha
Aidha amewataka wazazi kulipa
gharama hizo kwani kwa muhula ni sh 40,000 kwa watoto wa awali na
chekechea na kwa wanafunzi wa darasa la kwanza hadi lasaba ni sh
300,000 kwa mwaka ambapo chai mtoto anapewa bure
na chakula ambacho anapewa mchana ni wali , nyama , maharage, mboga
za majani na tunda .
kwa upande wake Fatuma Shaban
mpishi wa chakula shule yaskill path anasema pamoja na
jitihada mbalimbali zilizofanywa na uongozi wa shulehiyo
kuwashawishi wazazi watoe pesa za chakula lakini
wanagoma ni wazazi wachache ndio wanaona umuhimu na kulipia gharama
hizo nashindwa kuelewa sijui tatizo lipo wapi labda
hali ya uchumi ni mbaya au mwamko mdogo kwani ni
25% ya wanafunzi ndio wanaopata chakula shuleni.
“Roho inaniuma sana kama mzazi kuna
wakati naguswa na kuingiwa na huruma kama mzazi na uamua kuwasaidia
watoto ambao wanaanguka kwa njaa au utakuta mtoto mzazi aliwahi
kumlipia gharama za chakula lakini ghafla
anaamuakusitisha mwanae asile chakula , basi unakaona kanacheza
maeneo ya karibu na
unapotoa huduma ya chakula na kanawaangalia
wenzie wanavyokula hivyo inabidi umuite na
kumpatia chakula , wapo wazazi mnazungumza nao na anaomba umpatie
mwanae chakula kwa maelewano kuwa atalipa baada ya muda
flani lakini baadaye anageuka na kugoma kulipa gharama hivyo
hasara inabaki kwako inasikitisha sana ,”anasema Fatuma.
Mwanafunzi
wa shule ya msingi Majimaji Baraka Haule
anasema kutotolewa kwa chakula mashuleni kunawanyima
wanafunzi haki ya kusoma na kufanya vizuri kwenye masomo
kwani utakuta wanawaza chakula badala ya masomo na
kujisikia vibaya pindi wakiwaona wenzao wanavyokula na wengine
ujikuta vichwa vikiwauma kutokana na kutokula
Anasema kutokana na
kukosekana chakula shuleni baadhi yawanafunzi wamekuwa
wakipwwa pesa na wazazi wao ya kula chakula na wengine
hawapewi chochote na kusababisha waingie tamaa ya Kuiba, kufanya kazi
za kubeba tofali, kuvuna mahindi na kuosha vyombo majumbani kwa watu iliwapate
pesa ya kula na hivyo kukosa masomo.
Thomas Makwaya Mzazi anasema , kama
wapo wazazi wanaogoma kuchangia chakula wanakosea sana kwani
haiwezikani mtoto ashinde bila kula chochote tangu asubuhi hadi anaporudi
nyumbani kwani hata makuzi ya mtoto uwezo wa mtoto kuwa kiakili
inategemeana mlo kamili na vyakula mbalimbali vilevile ukuaji wa mwili
kiafya ni muhimu watoto wapate chakula bora ili kujenga kiakili na
kimwili.
kwa upande wake Mwalimu Nathan
Mtega wa shule yaMsingi Mitawa anasema swala
la chakula kwa watoto lipewe muhimu wa kipekee yeye anafundisha
watoto wa chekechea na wenye utindio wa ubongo wanatoka
kwenye shule ambazo awali milo mitatu hivyo
kula shuleni kunasaidia kupunguza utoro, kupenda kusoma kuwa mdadisi
na kujenga mwananfunzi "kukosekana chakula kunamuathiri mtotoanakuwa
siyo msikivu ana kosa raha , pia inavuja morali ya kufundisha kwa
mwalimu kwani huwezi kufundisha watoto wakiwa na njaa , hata ukitoa zoezi
watoto hawatafanya hivyo ni muhimu wazazi na viongozi
wa shule wakae na kujadili namna ya kumsaidia mtoto kupata
mlo shuleni kwani wapo wanafunzi wanaotoka kwenye familia maskini
hivyo kutolewa kwa chakula shuleni kunawasaidia kupata japo milo
miwili kwa siku hivyo kufanya vizuri kwenye masomo yao."anasema Nathan
Kwa upande wake Afisa
Elimu mkoa wa Ruvuma Ephaim Simbeye anasema mkoa wa Ruvuma
unashule 789 za msingi ambapo ni shule 347 pekee ndio zinazotoa
huduma yachakula shuleni ambapo watoto upatiwa kande au ugali ,
ambapo ameitaka jamii kuchangia chakula kwa hiari.
"Wazazi waelewe kuwa
kuchangia chakula ni muhimu na jukumu lao kwani ile
shea ya mtoto ambayo angekula nyumbani
anakula shuleni hivyo kumuondolea maradhi mbali mbali
ikiwemo vidonda vya tumbo kumshindiha mtoto bila kula chochote ni
ukatili mkubwa ",anasema Simbeye
Anasema kamati za
kukusanya chakula zishirikiane na kamati za wazazi kuhakikisha watoto
wanapata chakulashuleni kwani mkoa wa Ruvuma
una chakula kingi ni aibu watoto kushinda bila kula.
No comments:
Post a Comment