NA
MWAMVUA MWINYI,KIBAHA
MKUU
wa wilaya ya Kibaha ,mkoani Pwani ,Assumpter Mshama ameeleza iko haja ya kuwa
na usawa wa kijinsia kwa watoto wa kike na wa kiume pindi mwanafunzi wa kike
anapopata mimba akiwa shuleni, ili iwe fundisho kwa wanafunzi wengine .
Ameeleza,
inapaswa mtoto wa kike nae achukuliwe hatua sawa na mtoto wa kiume kwani
ujauzito hautokani na upande mmoja bali ni ushirika wa watu wawili wa jinsia
mbili tofauti.
Akizungumza
katika mahafali ya wanafunzi wa chuo cha ufundi stadi VETA Pwani, pamoja
na mambo mengine, Mshama alisema ifikie hatua kila mwanafunzi apate adhabu sawa
baada ya kupeana mimba ili kukomesha tabia hiyo.
“Kwa
wilaya hii wote mtapata adhabu, haiwezekani mtoto wa kike aendelee kutamba
wakati muda mwingine unakuta mtoto huyo ndio alikuwa chanzo cha kumtongoza
mwalimu au mwanafunzi mwenzie, hamjawahi kuona hilo!, Alihoji Mkuu huyo wa wilaya.
Aidha
Mshama alishauri Vijana hao waliomaliza chuo cha ufundi stadi VETA,
kujiajiri kwa kufungua viwanda vidogo vidogo na kutengeneza vifaa
vyenye ubora ili waweze kupambana na tatizo la ukosefu wa ajira.
Mapema
wakisoma risala yao mbele ya mgeni rasmi wanachuo ZAHARA ABDUL na IDD ATHUMANI
waliiomba serikali ya mkoa huo, kutoa kipaumbele cha ajira na fursa mbalimbali
zilizoko ndani ya mkoa.
Nae
kaimu mkuu wa chuo hicho, Karim aliainisha changamoto kubwa inayoikabili chuo
ni upungufu wa mabweni.
No comments:
Post a Comment