Meneja Mahusiano wa Shirika la Umeme nchini, (TANESCO), Leila Muhaji akizungumza na waandishi wa habari.
.....................................
Na. Farida Saidy, Morogoro.
Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO)
limewataka wananchi wanaofanya shughuli mbalimbali za kibinadamu jirani na
miundombinu ya umeme kuacha mara moja ili kujiepusha na madhara yatakayotokana
na mvua zinazoendelea kunyesha kwenye maeneo mbalimbali nchini.
Akizungumza na Mwandishi wa habari
hizi Kaimu Meneja Mahusiano TANESCO, Leila Muhaji amesema wale wote wanaojishughulisha
na shughuli mbalimbali za kibinadamu ikiwemo kuegesha magari, kulima, kujenga
makazi ya kuishi, na kufanya biashara katika miundombinu ya umeme wanatakiwa
kuacha.
Amewatahadharisha wananchi kutoshika
au kukanyaga nyaya za umeme zilizoanguka hususan katika kipindi hiki cha mvua.
“Ni vyema kutoa taarifa Tanesco
kitengo cha dharura kwa msaada zaidi,”alisema.
Katika hatua nyingine amesema kuwa
iwapo mvua itaambatana na radi au upepo mkali, umeme utapungua nguvu na
kuongezeka ndani ya nyumba hivyo wananchi wanashauriwa kuzima umeme kwenye
‘Main switch’, ili kuepukana na majanga yatokanayo na shoti ya umeme.
No comments:
Post a Comment