Pichani Zuhura Mizava mmoja wa wajumbe wa (UWT) Kibaha Vijijini akisaini karatasi ya kuchangia klabu ya soka ya Wanawake ya Mlandizi Queen's inayoshiriki Ligi kuu ya Wanawake, kulia ni Nahodha wa timu hiyo Wema Richard. Picha na Omary Mngindo.
Picha
ya kwanza Diwani wa Kata ya Mlandizi Kibaha Vijijini Mkoa wa Pwani Euphrasia
Kadala akisaini karatasi ya kuchangia klabu ya soka ya Wanawake ya Mlandizi
Queen's inayoshiriki Ligi Juu ya Wanawake, kushoto Nahodha wa timu hiyo Wema
Richard. Picha na Omary Mngindo.
........................................
Na
Omary Mngindo, Mlandizip
UONGOZI
wa klabu ya soka ya Wanawake ya Mlandizi Queen's inayoshiriki Ligi Kuu Tanzania
Bara ya Mlandizi Mkoa wa Pwani, umevamia Mkutano wa Jumuia ya Wanawake (UWT)
wilayani hapa wakihitaji ushirikiano wao.
Nahodha
wa timu hiyo Wema Richard akiambatana na mchezaji mwandamizi wa timu hiyo, Jamila
Hassan, Wema aliwaambia wana-UWT hao wa Kibaha Vijijini kwamba, timu yao ipo
kambini kwa muda mrefu na kwamba wanakabiliwa na changamoto mbalimbali.
Alisema
kuwa wanashiriki Ligi Kuu ya wanawake inayoshirikisha timu 12 kutoka mikoa
mbalimbali, ambapo katika kinyang'anyiro hicho pamoja na kupambana kuuwakilisha
Mkoa wa Pwani, wanakabiliwa na changamoto nyingi na kwamba wanahitaji
ushirikiano wa hali ya juu.
"Tulivyosikia
Mama zetu mpo hapa kwa ajili ya kikao cha kikazi, nasi watoto wenu tukaona
tutumie fursa hii kuja kuwataka muungane nasi kwa hali na mali katika ushiriki
wetu, kwani tunawawakilisha wanawake wote kuanzia hapa Mlandizi na Mkoa kwa
ujumla," alisema Wema.
Kwa
upande wake Jamila alisema kuwa ligi hiyo yenye ushindani wa hali ya juu,
pamoja na kupambana kwao lakini wanakabiliwa na ukata wa kifedha, hivyo
kuwaomba wana-UWT hao na wapenda michezo popote walipo wawaunge mkono katika hilo.
"Ligi
ya msimu huu yenye timu 12 inayochezwa nyumbani na ugenini, imekuwa na
ushindani wa hali ya juu, na kwamba tumecheza mechi 4, tumeshinda moja,
tumepoteza tatu, lakini tunawaahidi tutapambana kuhakikisha tunafanya vizuri
zaidi," alisema Jamila.
Mmoja
wa wana-UWT hao Salha Adinani amewapongeza kwa ushiriki wao, na kwamba kikubwa
wanatakiwa kuendelea kupambana katika ushiriki huo, huku akiwaomba wasichana
kujitambua katika mavazi.
No comments:
Post a Comment