NA
HADIJA HASSAN 18/12/2019 LINDI
Kamati
ya utekelezaji ya umoja wa vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Mkoa wa Lindi
imemsimamisha nafasi ya uongozi Rashidi Ally Mbumulile aliyekuwa mwenyekiti wa
umoja wa vijana Wilaya ya Nachingwea kwa tuhuma za kugushi umri wake.
Akizungumza
na waandishi wa habari katika ofisi za Makao makuu ya Chama cha mapinduzi Mkoa
wa Lindi Mwenyekiti wa umoja wa vijana UVCCM Majid Luponda jana alisema uamuzi
huo umekuja baada ya kamati hiyo kujiridhisha juu ya suala la kughushi umri kwa
mwenyekiti huyo kuwa mkubwa unaopata miaka 37.
Luponda
alisema kwa mujibu wa kanuni ya umoja wa vijana toleo la mwaka 2017 linamtambua
kijana ni Yule ambae amefikisha miaka 14 mpaka 35 “Kutokana na kanuni hii tunashauriwa
katika kuchagua ama kugombea katika nafasi yoyote ya uongozi, tunatakiwa
kumchagua kiongozi ambaye yuko chini ama miaka 30 ili anapofikia umri wa miaka
35 uwe ndio ukomo wa uongozi wake” alisema Luponda.
“Kwa
kutumia kanuni hiyo hiyo inatuelekeza kuwa endapo mtu anapokuwa ametoa taarifa
za uwongo hususani za kufoji umri na ikathibitika kuwa umri wake sio umri wa
kuwa katika kundi la umoja wa vijana itapelekea kufukuzwa moja kwa moja kwa
uongozi wake pamoja na kumuondoa katika kundi la vijana”
Luponda
alisema kutokana na hali hiyo kamati ya utekelezaji ya umoja wa vijana ya UVCCM
Mkoani humo inamsimamisha nafasi ya uongozi Mohamedi Mbumulile kwa muda
usiojulikana mpaka pale vikao vingine vya kitaifa vitakapokaliwa ili kutoa
maamuzi.
Pamoja
na mambo mengine Luponda pia alitumia fursa hiyo kutangaza ratiba ya mafunzo ya
ujasiriamali ambayo yanatarajiwa kufanyika katika Halmashauri zote za Mkoa wa
Lindi.
Alisema
mafunzo hayo yanatarajiwa kuanza tarehe 20/01/2020 hadi tarehe 31/01/2020
ambayo yataendeshwa na UVCCM kwa kushirikiana na TAEDO
No comments:
Post a Comment