Thursday, June 29, 2017
Wednesday, June 28, 2017
LOWASA AHOJIWA NA KUACHIWA.
Waziri Mkuu mstaafu, Edward Lowassa ameachiwa
kwa dhamana baada ya kuhojiwa kwa saa nne katika Ofisi ya Mkurugenzi wa
Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI).
Lowassa ameondoka makao makuu ya polisi saa
8.15 na kuelekea nyumbani kwake.
Akizungumza baada ya mahojiano hayo,
Mwanasheria wa Chadema, Peter Kibatala amesema Lowassa amejidhamini mwenyewe na
ametakiwa kuripoti tena Alhamisi saa 6.00 mchana.
Kibatala amesema Lowassa amehojiwa kwa kosa la
uchochezi na ameandika maelezo ya onyo juu ya kauli aliyoitoa wakati wa futari
iliyoandaliwa na mbunge wa Ukonga, Mwita Waitara.
“Mzee amehojiwa kwa kile wanachokiita kauli ya
uchochezi aliyoitoa Juni 23, mwaka huu wakati wa futari iliyoandaliwa na
Waitara. Baada ya kuhojiwa ameandika Maelezo ya Onyo na atatakiwa kuripoti tena
Alhamisi, Juni 29,” alisema.
Subscribe to:
Posts (Atom)