DIRA 2050 INA KINGA YA BUNGE -PROF MKUMBO
Na Mwandishi wetu SERIKALI imewatoa hofu Watanzania kuhusu hoja ya kuwa utekelezaji Dira 2050 unaweza kukumbwa na changamoto ya uhalali wa kisheria na hivyo mpango huo muhimu kwa taifa ukawa na ombwe la kiufanisi hapo baadae Akiongea katika kikao maalum na Wahariri kutoka jukwaa la Wahariri Tanzania TEF Waziri wa nchi ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaii Profesa Kitila Mkumbo amesema Dira ya taifa 2050 imewekewa ulinzi kwa kupelekwa bungeni na kwamba hakuna Rais atakayeweza kwenda kinyume na uamuzi huo Profesa Mkumbo amesema Dira 2050 itatekelezwa na Marais watatu,na kwa atakaetaka kuibadilisha atatakiwa kupeleka bungeni na kwamba Dira hii imekuwa tofauti kwa kuwa ya 2025 iliishia hatua ya kuidhinishwa na Baraza la Mawaziri tu. Waziri huyo amesema mchakato wa kutengeneza Dira 2050 umepitia hatua 13 ambazo ni kuandaa na kuidhinisha miongozo ya Dira. Mkakati wa kuandika Dira ulianza Aprili mwaka 2023, kwa kuunda vyombo vya kutathimini mchakato wa Dira na kufanya tathimini...