Posts

RAIS SAMIA AFANYA UTEUZI.

Image
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi kama ifuatavyo: Amemteua Prof. Mohamed Yakubi Janabi kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa   Muhimbili. Prof. Janabi alikuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI). Prof. Janabi anachukua nafasi ya Prof. Lawrence Maseru ambaye amestaafu. Amemteua Dkt. Peter R. Kisenge kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete. Dkt. Kisenge anachukua nafasi ya Prof. Janabi. Dkt. Kisenge ni Mkurugenzi wa Tafiti na Mafunzo wa (JKCI).    

DARAJA JIPYA LA WAMI KUANZA KUTUMIKA SEPTEMBA 30 MWAKA HUU 2022,

Image
  Katibu Wa Itikadi Na Uenezi CCM Ndg. Shaka Hamdu Shaka ,Wananchi na Baadhi ya Viongozi wa Chama Cha Mapinduzi wakipita katika Njia ya Watembea kwa miguu Kukagua maendeleo ya ujenzi wa daraja jipya la Wami ambalo ujenzi wake umefikia asilimia 89.02 na zaidi ya Sh. bilioni 75 zimepangwa kutumika. ..............................................   DARAJA Jipya la Wami lenye urefu wa mita 513.5 na barabara unganishi ya kilometa 3.8 litaanza kutumika Septemba 30, 2022.   Akizungumza katika ziara yake leo Septemba 18, 2022 Katibu, wa Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Shaka Hamdu Shaka amesema serikali imeridhishwa na ujenzi wa daraja hilo la Wami ambalo ujenzi wake umefikia asilimia 89 - "Daraja hili lilianza ujenzi mwaka 2018, hadi Rais Samia Suluhu Hassan anaingia madarakani ujenzi ulikua umefika asilimia 47, lakini ndani ya mwaka mmoja wa Rais Samia, kasi imeongezeka kwa asilimia 42 na sasa wataalamu wanatuambia ujenzi umefikia asilimia 89," ...