Monday, September 19, 2022

RAIS SAMIA AFANYA UTEUZI.

 No description available.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi kama ifuatavyo:

  • Amemteua Prof. Mohamed Yakubi Janabi kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa  Muhimbili. Prof. Janabi alikuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI).

Prof. Janabi anachukua nafasi ya Prof. Lawrence Maseru ambaye amestaafu.

  • Amemteua Dkt. Peter R. Kisenge kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete. Dkt. Kisenge anachukua nafasi ya Prof. Janabi. Dkt. Kisenge ni Mkurugenzi wa Tafiti na Mafunzo wa (JKCI).

 

 

No comments:

Post a Comment