Posts

WAZIRI MKUU ASEMA SERIKALI INABORESHA HUDUMA ZA AFYA NCHINI.

Image
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwapungia wananchi wa kijiji cha Lukozi wilayani Lushoto wakati alipowasili kijijini hapo akiwa katika ziara ya Mkoa wa Tanga, Oktoba 31, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) ...................................... WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali imedhamiria kuboresha huduma za afya kwenye maeneo mbalimbali nchini yakiwemo ya halmashauri ya wilaya ya Lushoto. Amesema lengo ni kuhakikisha kila kata inakuwa na kituo cha afya chenye uwezo wa kutoa huduma mbalimbali muhimu zikiwemo za maabara, upasuaji na mama na mtoto. Ametoa kauli hiyo leo (Jumatano, Oktoba 31, 2018) wakati akizungumza na wakananchi katika kata ya Malindi, baada ya kutembelea jengo la soko mbogamboga la Malindi. Waziri Mkuu amesema Serikali imejipanga vizuri katika sekta ya afya baada ya bajeti ya kununulia dawa kuongezeka kutoka sh. bilioni 31 kwa mwaka na kufikia bilioni 269. “Hatutaki tena kusikia mgonjwa anaenda hospitali na kukos...

WANANCHI WAMETAKIWA KUBADILI MFUMO WA MAISHA NA KUZINGATIA LISHE BORA

Image
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akipokea zawadi ya mbuzi kutoka kwa Diwani wa Kinyambuli Rubeni Charles wakati alipofanya ziara katika kijiji hicho ili kujionea hali ya ujenzi wa kituo pamoja na utoaji huduma za afya kijijini hapo. .......................................... Na WAMJW-MKALAMA,SINGIDA Watanzania kote nchini wametakiwa kufuata kanuni na taratibu bora za maisha ikiwemo kubadili mfumo wa maisha ili kuepuka kupata magonjwa yasiyo ya kuambukiza pamoja na udumavu kwa watoto wachanga. Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile katika Wilaya ya Mkalama Mkoa wa Singida wakati alipotembelea kituo cha afya na kuongea na wananchi. “Serikali chini ya uongozi wa Rais Magufuli inataka kila mtanzania awe na afya bora, ndo maana tunajitahidi kutoa elimu kwa umma kuhusiana na kutunza afya zenu ikiwemo kufanya mazoezi na kuepuka vyakula ...