Posts

SUBIRA MGALU ATOA AGIZO KWA TANESCO.

Image
  Naibu   Waziri wa Nishati, Subira Mgalu akizungumza na wananchi wilayani Bagamoyo kwa nyakati tofauti katika ziara yake ya siku mbili aliyoianza jana Tarehe 30 Desemba 2017 na leo Tarehe 31 Desemba 2017. ........................... Naibu   Waziri wa Nishati, Subira Mgalu amewataka mameneja wa Tanesco mikoa na wilaya kote nchini kuwaunganishia umeme wananchi wakaokuwa wameomba na kukamilisha malipo yao ndani ya siku saba tu. Agzo hilo amelitoa wilayani Bagamoyo alipokuwa katika ziara ya kukagua mradi wa kusambaza umeme vijijini REA awamu ya tatu unaotekelezwa nchi nzima. Alisema kila meneja wa TANESCO anatakiwa kuhakikisha kuwa, wateja wote waliojaza fomu na kukamilisha malipo yao wanatakiwa kuunganishwa umeme ndani ya siku saba tu ili kuondoa usumbufu kwa wananchi wa kusubiri kuunganishiwa umeme kwa muda mrefu. Aidha, alisema kufuatia agizo hilo atafanya ziara kwenye ofisi za TANESCO nchi nzima ili kuona idadi ya wananchi walioomba na kulipia hudu...

RC PWANI ATEMBELEA KIWANDA CHA BETRI KIBAHA.

Image
Mkuu wa Mkoa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo  jana Jumapili Tarehe 24 Desemba 2017. amekgua kazi ya ujenzi wa kiwanda cha kampuni ya China Boda Technical Group Ltd inayojenga kiwanda cha kutengeneza betri za magari katika Plot No 21 TAMCO Industrial Estate, Kibaha, Mkoa wa Pwani.  Mkuu huyo wa Mkoa wa Pwani amefanya ziara hiyo ili kukagua kasi ya ujenzi na kupokea changamoto zozote wanazokabiliana nazo ili kuona namna ya kushirikiana nao katika kuzitatua ili kufikia malengo. Katika ziara hiyo amefurahishwa na kasi ya ujenzi inavyoendelea na kusema kuwa ni ya kuridhisha. Aidha alipata fursa ya kuwasiliana kwa simu na Kandarasi wa Ujenzi huo ambaye amemuhakikishia kwamba ndani ya kipindi cha wiki mbili zijazo atakuwa amekamilisha kazi ya ujenzi kama mkataba wake unvyoonesha.  Alisema licha ya kazi nzuri inayoendelea katika kiwanda hicho bado kuna kazi kubwa ya ujenzi wa barabara kuingia kwenye kiwanda yenye upana wa meta 15 ambayo inatakiwa kujengwa na...

NAIBU WAZIRI NISHATI ASHANGAZWA NA TATIZO LA UMEME BAGAMOYO.

Image
Naibu waziri wa Nishati, Subira Mgalu amesema ameshangazwa na tabia ya kukatika umeme mara kwa mara katika wilaya ya Bagamoyo hali ya kuwa Serikali imeshaweka mikakati ya kuhakikisha umeme unakuwa wa uhakika. Naibu waziri huyo aliyasema hayo mjini Bagamoyo tarehe 24 Desemba 2017, alipokuwa akifunga maonesho ya wajasiriamali katika viwanja vya shule ya msingi Mbaruku. Alisema Serikali imeshaweka mikakati ya kuhakikisha umeme unakuwa wa uhakika nchi nzima ili kwenda sambamba na mahitaji katika kuelekea kuwa nchi ya viwanda. Aliongeza kuwa, katika mikakati iliyowekwa na serikali iliwahusisha mameneja nchi nzima ili nao waeleze changamoto zinazowakabili na hatimae kuzipatia ufumbuzi ili kuondokana na tatizo la kukatika umeme mara kwa mara. Alifafanua kuwa, ujenzi wa viwanda, wajasiriamali kujikwamua kiuchumi na maendeleo kwa ujumla vyote hivyo vinategemea upatikanaji wa umeme wa uhakika ili kufikia malengo. Alisema kutokana na mikakati hiyo anashangaa kuona mapak...

SUBIRA MGALU APONGEZA WANAWAKE BAGAMOYO.

Image
Mbunge wa viti Maalum Mkoa wa Pwani, Subira Mgalu ambae pia ni naibu waziri wa Nishati, (katikati) akiangalia bidhaa ya unga wa viazi vitamu unaotengenezwa na wajasiriamali wanawake Bagamoyo, wakati wa kufunga maonesho hayo yaliyofanyika uwanja wa Shule ya Msingi Mbaruku, wa kwanza kulia ni katibu tawala wa wilaya ya Bagamoyo, Erica Yegela, wa kwanza kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Bagamoyo, Fatuma Latu na wa pili kushoto ni Mwenyekiti wa Jukwaa la Uwezeshaji Wanawake Kiuchumi Bagamoyo, Teddy Alban Davis. ........................................... Mbunge wa viti maalum Mkoa wa Pwani, Subira Mgalu amepongeza jukwaa la Uwezeshaji Wanawake wilayani Bagamoyo kwa hatua waliyopiga katika kujikwamua kiuchumi. Subira Mgalu aliyasema hayo leo jumapili Desemba 24, 2017 wakati wa kufunga maonesho ya wajasiriamali yaliyoandaliwa na Jukwaa la Uwezeshaji Wanawake Kiuchumi Bagamoyo katika viwanja vya shule ya msingi Mbaruku. Alisema Jukwaa hilo limepiga hat...