Naibu
Waziri wa Nishati, Subira Mgalu akizungumza na wananchi wilayani Bagamoyo kwa nyakati tofauti katika ziara yake ya siku mbili aliyoianza jana Tarehe 30 Desemba 2017 na leo Tarehe 31 Desemba 2017.
...........................
Naibu
Waziri wa Nishati, Subira Mgalu amewataka mameneja wa Tanesco mikoa na
wilaya kote nchini kuwaunganishia umeme wananchi wakaokuwa wameomba na
kukamilisha malipo yao ndani ya siku saba tu.
Agzo hilo amelitoa wilayani Bagamoyo alipokuwa
katika ziara ya kukagua mradi wa kusambaza umeme vijijini REA awamu ya tatu
unaotekelezwa nchi nzima.
Alisema kila meneja wa TANESCO anatakiwa
kuhakikisha kuwa, wateja wote waliojaza fomu na kukamilisha malipo yao wanatakiwa
kuunganishwa umeme ndani ya siku saba tu ili kuondoa usumbufu kwa wananchi wa
kusubiri kuunganishiwa umeme kwa muda mrefu.
Aidha, alisema kufuatia agizo hilo atafanya ziara
kwenye ofisi za TANESCO nchi nzima ili kuona idadi ya wananchi walioomba na
kulipia huduma ya umeme na idadi ya waliounganishwa na kwamba meneja
atakaeshindwa kutekeleza hilo anapaswa kutoa maelezo juu ya kwanini mteja
hakuunganishiwa umeme ndani ya siku saba toka kulipia kwakwe.
Naibu waziri huyo wa Nishati amewataka Wananchi
waliopo kwenye vijiji vinavyopitiwa na mradi wa kusambaza umeme vijijini REA
wametakiwa kutumia fursa ya mradi huo kuchukua fomu na kulipia gharama ya
shilingi elfu ishirini na saba tu ili waunganishiwe umeme kupitia REA awamu ya
tatu.
Alisema Serikali imewathamini wananchi wake kwa
kuwepelekea mradi wa kusambaza umeme vijijini REA ili kila mwananchi apate
huduma hivyo ni matarajio ya serikali kuona fursa hiyo inatumika vizuri.
Kwa upande
wao wabunge wa jimbo la Bagamoyo na Chalinze wamempongeza Naibu waziri huyo wa
kwanza mwanamke katika wizara ya nishati kwa kujali wananchi na kuwatembelea
vijijini.
Dkt. Shukuru Kawambwa Mbunge wa Jimbo la Bagamoyo
amesema kufika kwa naibu waziri huyo vijijini kutampunguzia maswali anayoulizwa
na wananchi kuhusu vijiji ambavyo havijafikiwa na umeme.
Nae mbunge wa jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete
amesema wananchi wanajenga imani na serikali yao ya awamu ya tano hasa pale
wanpoona kiongozi kama Naibu waziri anawatembelea na kusikiliza vilio vya
wananchi
Alisema mfumo huo unawafanya wananchi kuimanini
serikali yao hasa pale ilani ya chama Cha mapinduzi inatekelezwa kwa vitendo.
Wakati huo huo Naibu waziri wa Nishati huyo
amewahakikishaia wananchi wa Kijiji cha Kongo kata ya Yombo wilayani Bagamoyo,
kuwa watapata umeme katikati ya januari 2018 ili kuwaondolea kero ya kukosa umeme
katika kijiji hicho kwa zaidi ya miaka 40 sasa.
Katika hatua nyingine Naibu waziri wa nishati
ambae ni Mbunge wa viti maalum Mkoa wa Pwani amechangia shilingi laki mbili
kwaajili ujenzi wa ofisi ya CCM katika kijiji cha Kongo kata ya Yombo wilayani
Bagamoyo.
Mradi wa kusambaza umeme vijijini REA awamu ya
tatu mzunguuko wa kwanza unatarajiwa kukamilika ifikapo Juni 2019 kwa kufikisha
umeme katika vijiji 3559 ambapo REA awamu ya tatu mzunguuko wa pili unatarajiwa
kuanza kutekelezwa 2019-2021 ili kutekeleza lengo la serikali la kuvipatia
umeme vijiji vyote 7873 vilivyobaki ifkapo mwaka 2021.
Naibu
Waziri wa Nishati, Subira Mgalu akizungumza na wananchi wilayani
Bagamoyo kwa nyakati tofauti katika ziara yake ya siku mbili aliyoianza
jana Tarehe 30 Desemba 2017 na leo Tarehe 31 Desemba 2017.
Naibu
Waziri wa Nishati, Subira Mgalu akitoa maelekezo kuhusu nguzo za umeme zilizokaa kwa muda mrefu katika kijiji cha Kongo kata ya Yombo wilayani Bagamoyo.
Naibu
Waziri wa Nishati, Subira Mgalu akipokea na kusoma mabango yaliyowasilishwa kwake na wananchi wa kijiji cha Kongo kata ya Yombo Halmashauri ya Bagamoyo wilayani Bagamoyo mkoa wa Pwani wakilalamikia kukosa umeme kwa zaidi ya miaka 40 sasa licha ya kuwa kijiji hicho ndicho chenye mtambo maji wa Ruvu chini.
Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu (katikati) akisikiliza maelezo ya kitaalamu kutoka kwa Msimamizi wa Miradi ya umeme vijijini REA Mkoa wa Pwani Mhandisi Mohamed Sauko (Kushoto) kushoto mwa Naibu waziri ni Meneja wa TANESCO wilaya ya Bagamoyo Daniel Michael Kyando, na kulia ni Mbunge wa Jimbo la Bagamoyo Dkt. Shukuru Kawambwa.
No comments:
Post a Comment