Posts

CCM YAITAKA SERIKALI KUCHUKUA HATUA MAUAJI YA PWANI.

Image
Chama Cha Mapinduzi kimeitaka Serikali kuchukua hatua za haraka kuhusu matukio ya Mauaji yanayoendelea katika Wilaya za Kibiti, Mkutanga na Rufiji Mkoani Pwani ili kuepusha mauaji hayo kuendelea kutokea.           Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, HUMPHEY POLEPOLE, amesema hayo Jijini Dar es salaam   leo wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mauaji yanayoendelea katika Wilaya hizo.           POLEPOLE pia amevitaka vyombo vya ulinzi na usalama kuhakikisha vinaelekeza akili, nguvu zao katika Wilaya hizo kwa kuwa maujia hayo yanasababisha kuzorota kwa shughuli za maendeleo.           Amesema chama kwa muda mrefu kimekaa kimya kikiamini hatua zitachukuliwa kwa kuwa wanachama wake na watendaji wameendelea kupoteza maisha ambapo amesema kwa sasa imetosha. Kuhusu suala la uchaguzi ambao unaendelea ndani ya Chama hicho...

KIBAHA YAZINDUA JUKWAA LA UWEZESHAJI WANAWAKE KIUCHUMI

Image
Mkuu wa wilaya ya Kibaha ,Assumpter Mshama na mbunge wa viti maalum mkoani Pwani Subira Mgalu mwenye kiremba cha blue wakitembelea mabanda mbalimbali ya bidhaa za wajasiriamali wa Mji wa Kibaha ,baada ya kuzindua jukwaa la wanawake la kuwawezesha kiuchumi mjini hapo .(picha na Mwamvua Mwinyi ) .................... WILAYA ya Kibaha imezindua jukwaa la uwezeshaji wanawake kiuchumi na kuchagua viongozi wake watakaoongoza katika kipindi cha miaka mitano. Jukwaa hilo limempitisha Betty Msimbe kuwa mwenyekiti huku Sada Duda akichaguliwa katibu kipindi hicho . Afisa maendeleo ya jamii halmashauri ya Mji wa Kibaha ,Leah Lwanji aliwataja viongozi hao ambao wamechaguliwa na akina mama wajasiriamali mbalimbali . Alieleza kuwa kuundwa kwa jukwaa hilo kutasaidia kuwezeshwa vikundi vya akinamama wajasiriamali kirahisi . Leah alisema wanawake waungane waache kujiweka binafsi ili kupiga hatua kimaendeleo na kiuchumi . Hata hivyo alisema ,katika kipindi cha mwezi ...

YANGA YAPOKELEWA KWA SHANGWE BUNGENI LEO MAY 25, 2017.

Image
Mabingwa wa Ligi kuu Tanzania Bara Dar Young African “Yanga” kwa msimu 2016/2017 wakifurahia na mawaziri na wabunge mara baada ya kulileta kombe la Ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara Bungeni Mjini Dodoma.   Mabingwa wa Ligi kuu Tanzania Bara Dar Young African “Yanga” kwa msimu 2016/2017 wakifuatilia mijadala mbalimbali Bungeni Mjini Dodoma. Timu ya Mpira ya Mbao FC kutoka Mwanza wakifuatilia mijadala mbalimbali Bungeni, Mbao Fc wapo Mjini Dodoma kwa ajili ya maandalizi ya Mchezo wa fainali za FA kati yao na Simba Fc zitakazofanyika katika Uwanja wa Jamhuri Mjini Dodoma Jumamosi ya May 27, 2017.   Mbunge wa kuteuliwa Mhe. Abdallah Bulembo akiuliza swali katika kikao cha thelasini na nne cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 25, 2017. Mbunge wa Mbulu Vijijini Mhe. Flatei Massay akiuliza swali katika kikao cha thelasini na nne cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 25, 2017.   Waziri wa Mambo ya Nda...