Posts

BONDIA THOMAS MASHALE ADAIWA KUUWAWA DAR ES SALAAM.

Image
Bondia mtanzania Thomas Mashali maarufu kama (Simba Asiyefugika), amekutwa amekufa huku akiwa na majeraha  usiku wa kuamkia leo huko maeneo ya Kimara jijini Dar es salaam kutokana na sababu ambazo hazijajulikana mpaka sasa. Kwa mujibu wa katibu mkuu wa Oganization ya ngumi za kulipwa nchini PST Antony  Lutta, amesema kuwa taarifa walizozipata ingawa bado  hazijathibitishwa inaonyesha Thomas Mashali ameuwawa. Lutta ameongeza kwamba marehemu enzi za uhai wake amekuwa na tabia ya kufanya vurugu akiwa amelewa sasa hatujui nini kimempata ambapo  mwili wake umekutwa maeneo ya Kimara jijini Dare s salaam ukiwa na majeraha baada ya hapo  ulichukuliwa na kupelekwa kuhifadhiwa katika  hospitali ya taifa muhimbili. Marehemu Mashali kabla ya kifo chake alikuwa  acheze na bondia Chimwemwe kutoka nchini Malawi ,pigano ambalo lilipangwa kufanyika mkoani  morogoro siku ambayo bondia mwenzake Dullah Mbabe alipangwa kucheza pigano la utangulizi. ...

DC. KONGWA AZINDUA KAMPENI YA ONDOA NJAA KONGWA (ONJAKO).

Image
Mkuu wa wilaya ya Kongwa Mh Deo Ndejembi akizindua kampeni ya kuondoa Njaa wilaya ya Kongwa, (ONJAKO)   Mkuu wa wilaya ya Kongwa Mh Deo Ndejembi akizungumza mara baada ya kuzindua kampeni ya kuondoa Njaa wilaya ya Kongwa, (ONJAKO)  ........................................... Mkuu wa Wilaya ya Kongwa Mkoani Dodoma Mhe Deo Ndejembi ameanzisha kampeni ya kuondoa Njaa wilaya ya Kongwa, (ONJAKO) yenye dhamira ya kuwasaidia wananchi kuondokana na hali yanjaa ambayo ni kadhia kubwa katika maeneo mbalimbali ya Wilaya hiyo sambamba na Taifa kwa ujumla. Kuanzishwa kwa Kampeni ya Okoa njaa Wilaya ya Kongwa imejili wakati Mkuu huyo wa Wilaya ya Kongwa Akizungumza na Wakuuwa Idara na vitengo, Madiwani wa Kata zote zilizopo Wilayani humo, Watendaji wa Kata, Maafisa Tarafa, Waratibu Elimu Kata, Wenyeviti wa Vijiji vyote 87 vya Wilaya ya Kongwa na watendaji wao, pamoja na wadau waalikwa na Kilimo. Akizindua kampeni hiyo Dc Ndejembi alisema kuwa Kampeni h...

DC. MUHEZA,HAJAT, MHANDISI, MWANAASHA TUMBO, ATEMBELEA ZAHANATI MPYA YA KIJIJI CHA ZENETI

Image
 Mkuu wa wilaya ya Muheza,Haja Mhandisi,Mwanasha Tumbo katika akiongozwa na Diwani wa Kata ya Potwe,Rashid Mdachi na Mwenyekiti wa Serikali ya  Kijiji cha Zeneti wakitembelea Jengo jipya la Zanahati ya Zeneti iliyojengwa kwa ushirikiana baina ya Halmashauri,Wananchi na Shirika la World Vision na Mbunge wa Jimbo hilo ambalo limegharimu kiasi cha milioni 35.2.   Kulia ni Kaimu Mganga Mkuu wa Wilaya ya Muheza,Mathew Mganga akimuongozwa Mkuu wa wilaya ya Muheza, Hajat, Mhandisi Mwanasha Tumbo aliyetembelea zahanati ya Zeneti kuona jinsi inayoendelea na ujenzi wake kushoto ni Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji cha Zeneti   Kaimu Mganga Mkuu wa wilaya ya Muheza,Mathew Mganga kulia akisisistiza jambo kwa Mkuu wa wilaya ya Muheza,Hajat Mhandisi Mwanasha Tumbo wa pili kutoka kushoto kuhusu ujenzi wa zahanati hiyo katikati ni Diwani wa Kata ya Potwe,Rashid Mdachi.   Diwani wa Kata ya Potwe,Rashid Mdachi akimuonyesha kitu Mkuu wa wilaya y...