Kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya wadhamini
ya shule za Yemen Hassan Akrabi, katikati ni Mgeni rasmi katika mahafali hayo
Mwenyekiti wa Bodi ya wadhamini wa Baraza la wakuu wa shule za Kiislamu
Tanzania, Ansaar Abubakar Kachwamba na kulia ni Mkuu wa shule ya Sekondari
Yemen, mwalimu Hamisi Togwa.
Mgeni rasmi katika mahafali hayo Mwenyekiti wa
Bodi ya wadhamini wa Baraza la wakuu wa shule za Kiislamu Tanzania, Ansaar
Abubakar Kachwamba akizungumza katika mahafali hayo ya tisa yaliyofanika
viwanja vya shule za Yemen Chang'ombe jijini Dar es Salaam.
...............................
Vijana wanaohitimu katika shule za kiislamu hapa
nchini wametakiwa kuendeleza maadili mema waliyopata katika shule hizo ili
kuujengea heshima uislamu.
Akizungumza katika mahafali ya tisa ya shule ya
sekondari Yemen, Mgeni rasmi katika mahafali hayo, Ansar Abubakar Kachwamba
alisema jamii imejenga imani kubwa kwa shule za kiislamu na waislamu kwa ujumla
hivyo ni jukumu la vijana wanaohitimu katika shule za kiislamu kuilinda heshima
hiyo mbele ya jamii.
Ansaar Kachwamba, ambae ni Mwenyekiti wa Baraza
la wakuu wa shule za kiislamu hapa nchini alisema maadili mema yametoweka
katika jamii hivyo shule za kiislamu ambazo miongoni mwa majukumu yao ni kusimamia maadili kwa vijana
zinapaswa kuungwa mkono na kila mtu na kwamba vijana wanaohitimu katika shule
hizo wanapaswa kuwa mstari wa mbele katika kusimamia na kudumu katika maadili
mema.
Aidha, aliwataka wazazi kutoa ushirikiano kwa
walimu ili kujenga timu moja inayoweza kusimamia taaluma na maadili kwa vijana
na kwamba kazi hiyo wasiachiwe walimu peke yao.
Alisema kazi ya kukuza taaluma na kusimamia
maadili sio ya walimu peke yao bali ni ushirikiano kati ya mzazi, mwalimu,
mtoto pamoja na jamii kwa ujumla kwakuwa faida ya kuwa na maadili mema ni ya
Taifa kwa ujumla na sio ya mtu moja.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya shule za
Yemen, Hassan Akrabi aliwataka wazazi kuhakikisha wnalipa ada kwa wakati ili
kuiwezesha shule kupiga hatua katika mambo na mikakati mbalimbali waliojiwekea
ikiwemo kukuza taaluma shuleni hapo.
Alisema mikakati nayopangwa na shule haiwezxi kufanikiwa
ikiwa wazazi hawatoi ushirikiano haswa katika swala la ulipaji wa ada.
Akisoma risala mbele ya mgeni rasmi Mkuu wa shule
hiyo Hamisi Togwa alisema shule hiyo ni miongoni mwa shule wastani wa kati hapa nchini na kwamba imeendelea kufanya
vizuri kitaaluma tangu kuanzishwa kwake.
Alisema shule hiyo imefanikiwa katika kupunguza
idadi ya wanafunzi wanaopata daraja la nne huku ikihuisha na kuendeleza darsa
la Qur ani pamoja kukuza elimu ya kiarabu.
Akizungumzia changamoto zinazoikabili shule hiyo,
mwalimu Togwa alisema ni pamoja na kupanda kwa gharama za uendeshaji hali
inayopelekea kupanda kwa ada ili kukabiliana gharama za uendeshaji.
Aidha, alisema mikakati ya shule hiyo ni
kuhakikisha inaongeza ufaulu kwa madaraja ya kwanza hadi la tatu na kuondoa au
kupunguza idadi ya wanafunzi wanaopata daraja la nne na sifuri.
Jumla ya wanafunzi 91 wamehitimu elimu ya kidato
cha nne katika shule ya sekondari Yemen mwaka huu wa 2017 ambao kati yao wavulana 45 na wasichana ni 46
.
Mwenyekiti wa Bodi ya wadhamini ya shule za Yemen
Hassan Akrabi, akizungumza katika mahafali hayo.
Meneja wa shule za Yemen, Jamila Awadhi,
akizungumza katika mahafali hayo.
Baadhi ya wanafunzi waliomaliza katika shule hiyo
ya Yemen ambao kwa sasa wanasoma katika vyuo vikuu mbalimbali walipojumuika na
wadogo zao katika mahafali hayo.
Kiongozi wa wanafunzi waliomaliza shuleni hapo
miaka ya nyuma ambao kwa sasa wanasoma katika vyuo vikuu, Salim Saidi Salim
akitoa nasaha zake kwa wahitimu wa kidato cha nne 2017 katka mahafali hayo
yaliyofanyika viwanja vya za Yemen Chang'ombe jijini Dar es Salaam.
Wahitimu wa kidato cha nne shule ya Sekondari
yemen jijini Dar es Salaam wakiwa kwenye mahafali yao.
No comments:
Post a Comment