Mashndano ya Kombe la Mazingira Kabumbu cup 2017
Wilayani Bagmoyo yamefungwa rasmi jna katika uwanja wa Mwanakalenge mjini Bagamoyo.
Katika mechi ya kufunga mashindano hayo
iliyochezwa kati ya timu bingwa ya Halmashauri ya Chalinze Pera FC. na timu
bingwa ya Halmashauri ya Bagamoyo ya Nianjema FC. timu ya Pera iliibuka na ushindi
wa mabao 2-1 dhidi ya wenyeji Nianjema.
Katika mchezo huo timu zote zilionyesha uwezo
wake uwanjani ambapo dakika ya 8 mchezaji Nyange Kabulu aliipatia timu ya Pera
bao la kwanza ambapo bao hilo lilidumu mpaka dakika ya 36 timu ya Nianjema
iliposawazisha kupitia mchezaji wake Mwinyi Gandi.
Wakati mchuano ukionekana kuwa mkali kwa timu
zote mbili dakika ya 55 timu ya Pera FC. ilijipatia bao la pili kupitia mchezaji
wake Rajabu Jongo ambapo mpaka mwisho wa mchezo Pera Fc imetoka na ushindi wa
mabao 2-1 dhidi y wenyeji Nianjema FC.
Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo, Alhaj, Majid Mwanga
alizipongeza timu zote kwa kushiriki vyema katika mashindano hayo na kuwataka
kuendeleza umoja na mshikamano katika mambo mbalimbali ikiwemo usafi wa
mazingira ambao ndio lengo la kuanzisha mashindao hayo.
Awali ilichezwa mechi ya ufunguzi kati ya kamati
ya ulinzi na usalama ya wilaya ya Bagamoyo na madiwani wa Halmashauri zote
mbili ambapo timu ya kamati ya ulinzi na usalama iliibuka na ushindi wa mabao
2-1
Katika mechi hiyo ya ufunguzi bao la kwanza la
kamati ya ulinzi na usalama lilifungwa na askari polisi Samweli huku bao la pili likiwa limefungwa na askari
magereza Yohana huku bao la upande wa madiwani likiwa limefungwa na Diwani wa
kata ya Bwilingu Lukasi Lufunga.
Akizungumza mara baada ya kumalizikia kwa mchezo
huo, mbunge wa jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete aliipongeza timu ya Pera kwa
kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 licha ya kuchezea ugenini na kuwataka waendeleze
uwezo walionao ili kukuza vipaji vya vijana katika swala la michezo na hatimae
Chalinze iweze kutoa wachezaji bora zaidi.
Aidha, kufuatia ushindi waliopata timu ya Pera
FC. Mbunge Ridhiwani kikwete aliwazawadia pesa taslimu shilingi laki moja na
nusu wachezaji wa timu ya pera huku laki moja akiitoa kwa wachezaji wa timu ya
Nianjema.
Kikosi cha timu ya Pera FC. kilikuwa na wachezaji
1. Shekhe Natori
2. Chama Iddy
3. Mogela Nahau
4. Gaudensi Maarifa
5. Chujo Joseph
6. Shaibu Jongo
7. Njechele Nyang'anyi
8. Rajabu Jongo
9. Juma Mfu
10. Hassan Waziri
11. Nyange Kabulu
Kwa upande wa Nianjema FC kikosi kilikuwa ni
1. Karimu kiga
2. Ally kibinda
3. Ismail Chachupa
4. Issa Kanali
5. Mtumwa Ally
6. Yasini Kinala
7. Mwinyi Gandi
8. Diksoni Chagulo
9. salehe Masegele
10. Ibrahimu Masudi
11. Eliasi Boazi
Wachezaji na mashabiki wa timu ya Pera FC.
wakifurahia ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Nianjema FC.
Mchezaji wa timu ya Pera FC akijaribu kuwatoka
wachezaji wa timu ya Nianjema FC.
Wachezaji wa akiba, Viongozi na Mashabiki wa timu
ya Nianjema FC. wakishikwa na butwaa baada ya kufungwa goli la pili.
Mshambuliaji wa timu ya Nianjema FC akijaribu
kuwatoka wachezaji wa Pera FC.
Baadhi ya wachezaji wa timu ya kamati ya ulinzi
na usalama wilaya ya Bagamoyo wakiongozwa na Mkuu wa wilaya hiyo Alhaj, Majid Mwanga
wakifuatilia pambano hilo.
Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo, Alhaj, Majid Mwanga
wapili kushoto na Mbunge wa jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete wa pili kulia wakiwa
na nyuso za furaha mara bada ya mpira kumalizika
No comments:
Post a Comment