Tuesday, November 21, 2017

WAZIRI WA NISHATI ATEMBELEA KIWANDA CHA NGUZO ZA UMEME BAGAMOYO.



Waziri wa Nishati, Dkt. Merdard Kalemani (katikati)  alipowasili katika Kiwanda cha kutengeneza nguzo za umeme ambazo zinatengenezwa kwa kutumia zege.

Kiwanda hicho kinachojulikna kwa jina la East Africa Infrastructure Engineering Limited, kipo kijiji cha Kidomole kata ya Fukayosi Halmashauri ya Bagamoyo wilaya ya Bagamoyo Mkoani Pwani.

Sehemu ya nguzo zinazozalishwa na kiwanda cha East Africa Infrastructure Engineering Limited, nguzo hizo zinazalishwa kwa kutumia zege na hutumika kusambazia umeme badala ya kutumia nguzo za miti ambazo hazidumu kwa muda mrefu.
 Waziri wa Nishati, Dkt. Merdard Kalemani wa kwanza kulia akipata maelezo kutoka kwa mtaalamu wa kiwandaa hicho, wapili kulia ni Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo, Majid Mwanga, wa tatu kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Kiwanda hicho cha East Africa Infrastructure Engineering Limited, Otieno Igogo.

Mwenyekiti wa Bodi ya Kiwanda cha East Africa Infrastructure Engineering Limited, Otieno Igogo, kulia, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Bagamoyo, Fatuma Latu, na Mbunge wa jimbo la Bagamoyo Dkt. Shukuru Kawambwa wakifurahia jambo katika kiwandaa hicho.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Bagamoyo, Ally Ally Issa kulia akibadilishana mawazo na Katibu Mwenezi wa CCM wilaya ya Bagamoyo,  John Francis maarufu kama Bolizozo walipokuwa katika kiwanda hicho kumsubiri Waziri wa Nishati.
  Waziri wa Nishati, Dkt. Merdard Kalemani, kulia akiagana na Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo Majid Mwanga mara baada ya kumaliza ziara yake ndani ya kiwanda hicho.

No comments:

Post a Comment