Baadhi ya wakaanga samaki katika soko la samaki
mjini Bagamoyo wamelalamikia kuondolewa kwa kwenye maeneo yao na kusema eneo
eneo walilohamishiwa halitoshi kwa shughuli zao.
Wakizungumza na Mwandishi wa habari hizi katika
soko la samaki mjini Bagamoyo wakaangaji hao walisema wameshahamishwa mara
mbili sasa na kwamba hawana tena pesa za kujengea sehemu nyingine.
Walisema awali walibomolewa vibanda vyao na
kutakiwa kuhamia sehemu nyingine ambayo nayo wameambiwa waondoke.
wakionekana
kukerwa na kitendo hicho walisema sehemu ambayo kwa sasa wapo na
kutakiwa kuondoka wapo jirani na eneo linalomilikiwa na mzungu hali
inayowafanya wajione wanyonge wanaondolewa ili aachwe mzungu hali ya kuwa
mabanda yao hayaingiliani na eneo la mzungu.
Diwani wa kata ya Dunda mjini bagamoyo Dcksoni
Makamba alisema ni kweli wananchi hao wanaofanya shughuli zao za kukaanga
samaki waliondolewa kwa sababu ya upanuzi wa ujenzi wa soko la kudumu la
kukaangia samaki.
Aidha, Makamba alisema sehemu waliyopo kwa sasa
ipo jirani na eneo linalomilikiwa na mzungu ambalo kiusalama ni hatari kuwepo
hapo kutokana na shughuli zao za moto hali inayoweza kusababisha ajali ya moto
kwenye majengo mengine.
Diwani huyo aliwataka wananchi hao kuwa na subira
wakati uongozi wa halmashauri ukishughulikia umaliziaji wa soko la kudumu la
kukaanga samaki ambalo kila mmoja atakuwa kwenye chumba chake na kutumia majiko
ya gesi.
No comments:
Post a Comment