Waombaji wa nafasi za Jeshi la Kujenga Taifa wakiwa Ofisi ya Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo kusubiri hatima ya maombi yao katika usaili ambao ni vijana 65 tu ndio wanaohitajika.
Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo, Alhaj, Majid Mwanga, akizungumza na waandishi wa Habari wakati wa usaili kwa vijana walio omba nafasi za JKT. wilayani humo.
..............................................
Vijana wilayani bagamoyo wametakiwa kujenga tabia
ya kujitolea katika shughuli mbalimbali za kijamii ili kujenga uzalendo na nchi
huku wakitarajiwa kuwa wao ndio viongozi wa baadae.
Wito huo umetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo,
Majid Mwanga alipokuwa akizungumza na vijana walio omba nafasi za kujiunga JKT mwaka
2017 katika usaili uliofanyika ofisi za Mkuu wa wilaya hiyo.
Alisema wilaya ya Bagamoyo imepewa nafasi 65 tu
huku waombaji wakiwa 1,175 idadi kubwa ukilinganisha na miaka iliyopita.
Aliongeza kwa kusema kuwa kutokana na idadi hiyo
kuwa kubwa ni wazi kuwa vvijana wengi watakosa nafasi hizo na kuwataka kubaki
tabia hizo za kujitolea kama ambavyo wangeingia JKT.
Akizungumzia fursa zinazoweza kupatikana katika
kujitolea ni pamoja na kuanzisha kilimo cha Muhogo na Mpunga
kitakachowashirikisha vijana wote waliokosa nafasi za JKT wilayani Bagamoyo ili
kuzalisha Muhogo na Mpunga na hatimae kuuza kuwa ni njia ya kujiongezea kipato
kutokana na mazao hayo ya kilimo.
Alisema mpango huo utaanza mara moja na kwamba
tayari heka 50 za kulima muhogo na heka 50 za kulima mpunga zimepatikana
wilayani Bagamoyo lengo likiwa ni kujenga tabia ya kujitolea na kuwawezesha
vijana kuwa na uwezo wa kubuni miradi itakayowasadia kujipatia kipato na
kuongeza kuwa hiyo ni moja ya ajira.
Akizungumzia zao la muhogo alisema muhogo
unahitajika sana nchini Oman na kwamba kutokana na mahusiano mema yaliyopo kati
ya oman na Tanzania fursa ya kupeleka muhogo nchini Oman ipo kinachotakiwa ni
kuzalisha kwa wingi zao la muhogo.
Aidha, aliongeza kwa kusema kuwa, katika
kuhakikisha mpango huo unakuwa na manufaa asilimia tano inayotengwa kwenda kwa
vijana inaweza kupelekwa kwa vijana hao watakaojitolea kulima Muhogo na Mpunga
ili ziasidie katika uendeshaji wa kilimo hicho.
Kwa upande wao vijana waliozungumza na
bagamoyokwanza blog walisema wamejitolea kuingia JKT bila ya malipo wakitaraji
kuwa kujitolea kwao kutazaa matunda kwa siku za usoni na kwamba wazo la mkuu wa
wlaya kuwapeleka kwenye kilimo watakaokosa nafasi ni wazo zuri kwakuwa litawafanya
waonekane ni vijana wanaoweza kujitolea na hivyo ni rahisi kupata fursa
nyingine zitakazojitokeza kwa siku za usoni.
walisema wengi hushindwa kulima kutokana na
changamoto za kumudu gharama za kilimo cha uhakika, pembejeo na maeneo muafaka
kwa kilimo kinachokusudiwa ambapo walisema kupitia mpango huu wa Mkuu wa wilaya
wanaamini changamoto hizi zitapatiwa ufumbuzi na hatimae kufanikiwa kupitia
kilimo.
Walisema licha ya kilimo hicho kutajw kuwa ni cha
umoja lakini kupitia mpango huo kila mmoja atapata elimu juu ya uendeshaji wa
kilimo, namna ya kukabiliana na changamoto hali itakayopelekea kupata ujuzi wa
kuendesha shamba hata mtu akiwa peke yake.
No comments:
Post a Comment