Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo, Alhaj Majid Mwanga,
akikagua godaoni la Korosho lilipo kata ya Fukayosi Halmashauri ya Bagamoyo
ambapo Godaoni hili mpaka sasa limekusanya Tani 48 kutoka kwa wakulima
zikisubiri siku ya mnada.
Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo, Alhaj Majid Mwanga
amefanya ziara ya kukagua magodaoni ya korosho wilayani Bagamoyo na kubaini
ongezeko la zao la korosho ukilinganisha na mwaka 2017.
Mkuu huyo wa wilaya amewataka wakulima wa korosho
wilayani Bagamoyo kuzikusanya korosho zao kwenye magodaoni yaliyotengwa kwenye
kila kata ili ziuzwe kwenye mnada wa serikali.
Aidha, ameonya wale wote watakaouza nje ya mnada
kwamba korosho hzo zikikamatwa zitataifishwa na kuwa mali ya sehemu
iliyokamata.
Alisema kuuza korosho nje ya mnada kunaipunguzia
Halmashauri ruzuku ya upatikanaji wa pembejeo ambazo zinatolewa kulingana na takwimu
ya mauzo ya kwenye mnada.
Amewataka wananchi kutoa ushirikiano kuhakikisha
hakuna walanguzi wanaokuja kununua korosho nje ya mnada ili kuiongezea korosho
thamani na hataimae mkulima afaidike na kile alichokivuna.
Nae Mwenyekiti wa Halmashauri ya Chalinze Saidi
Zikatimu aliwataka wananchi kuimarisha kilimo cha Korosho kwani ni zao ambalo
linaiingizia serikali mapato na kukuza pato la mkulima kulingana na be yake
kuwa juu kwa sasa.
Alisema kulingana na thamani ya korosho, Korosho
kwa sasa inajulikana kama Dhahabu ya kijani hivyo kila wananchi wanapaswa
kupanda miche mipya ya korosho badala ya kutegemea ile iliyopandwa zamani.
alisema agizo la serikali kila kaya inapaswa
kupanda miche 30 huku kijiji kikitakiwa kupanda miche elfu tano.
Kwa upande wao wakulima wa Korosho wilayani
Bagamoyo walisema changamoto inyowakabili ni kuchelewa kwa mbolea ambapo mbolea
inaletwa wakati tayari maua yameshatoka na hivyo ni vigumu kuwazuia wadudu
wanaoshambulia zao hilo la korosho.
Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo, Alhaj Majid Mwanga, akikagua godaoni la Korosho la kata ya Kiwangwa, kulia ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Chainze, Saidi Zikatimu wa pili kushoto ni Diwani wa kata ya Kiwangwa, Malota husein Kwaga, mpaka sasa tani tisa zimekusanywa kijiji cha Kiwangwa.
Maafisa Kilimo, Ushirika, wa Halmashauri ya Chainze, wakijadili jambo wakati wa zoezi la kukagua magodaoni ya Korosho.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Chainze, Saidi Zikatimu akizungumza na wakulima wa Korosho katika kijiji cha visezi kata ya Vigwaza Halmashauri ya Chalinze wialayani Bagamoyo.
No comments:
Post a Comment