Kikundi cha sanaa za maigizo cha Kale Leo Sanaa
Network kimefanya onyesho lake la pili
katika chuo cha cha sanaa Bagamoyo, kinachojulikana kwa jina la Taasisi ya
Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) na kuonyesha umahiri wake katika fani ya
maigizo.
Akizungumza na bagamoyokwanza blog, Muongozaji wa
kikundi cha Kale Leo Sanaa Network, Ghoche Materego alisema kikundi hicho
kinajumuisha wasanii wakongwe na wa sasa wengi wao wakiwa wamepata Elimu yao
Taasisi ya Sanaa Bagamoyo (TaSUBa) lengo likiwa kukuza taaluma ya sanaa na
kuonyesha maisha halisi ya wanadamu katika jamii kupitia sanaa ya maigizo.
Alisema Kikundi hicho kinapenda kutoa maigizo ya
kuwaenzi mashujaa katika ukanda huu wa Afrika Mashariki na kati ili kizazi
kinachokuja kisipoteze historia ya mashujaa ambao kwa namna moja wamefanya
juhudi katika kupigania haki mbalimbali za kibinadamu na kujitawala.
Katika igizo liliwavuta wengi ni lile linaloitwa Mfumo liongo, ambapo Mfumo Liongo alikuwa
ni mtu mashuhuri na shujaa aliyeishi karne ya 15 katika Pwani ya Afrika
Mashariki na kwamba Historia yake itaendele kukumbukwa.
No comments:
Post a Comment