Mganga
Mkuu wa Serikali Prof. Bakar Kambi akisisitiza jambo wakati wa Semina ya
uhamasishaji wa wahariri na wakuu wa Idara ya Afya juu ya magonjwa yaliyokuwa
hayapewi kipaumbele ilofanyika mapema leo katika ofisi za Wizara ya Afya jijini
Dar es salaam, pembeni yake ni Dkt. Janeth Mgamba
...........................................
NA WAMJW-DAR ES SALAAM.
SERIKALI kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia , Wazee na
Watoto imefanikiwa kudhibiti magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele kwa
asilimia 90 kupitia mpango wa kudhibiti magonjwa hayo hapa nchini NTD.
Hayo yamezungumzwa na Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Bakari Kambi
wakati alipofungua semina ya uhamasishaji wa kupambana na magonjwa hayo kwa
wahariri wa vyombo vya habari na Wakuu wa idara mbalimbali wa Wizara ya Afya
leo jijini Dar es salaam.
“Tumepata mafanikio kwani mpaka kufikia Oktoba 2017 huu
tumefanikiwa kupunguza ugonjwa wa matende na mabusha katika wilaya
95 sawa na asilimia 77 kati ya wilaya 120 na hivyo tumesitisha kutoa dawa
katika wilaya hizo” alisema Prof. Kambi.
Aidha Prof. Kambi amesema kuwa katika mafanikio hayo pia Serikali
imefanikiwa kupunguza maambukizi ya ugonjwa wa Vikope (Trakoma) katika wilaya
58 sawa na asilimia 82 kati ya wilaya 71 hapa nchini.
Kwa mujibu wa Prof. Kambi amesema kuwa kwa maeneo ya nyanda za juu
hususan katika maeneo ya Rungwe,Kyela,ileje na Busekeleo wamefanikiwa
kupima wananchi na kuonyesha kuwa maambukizi yamepungua na hivyo kuendelea
katika wilaya zilizobaki.
Kwa upande wake Mratibu wa Kitaifa wa Mpango wa kupambana na
Magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele Dkt. Upendo mwingira amesema kuwa
wanajamii wanatakiwa wajitokeze katika kupata dawa za kujikinga na magonjwa hayo
kwani muitikio ni mdogo na inaweza kusababisha madhara makubwa siku za usoni.
Aidha Dkt. Mwingira amesema kuwa Semina hiyo imelenga kuwaelimisha
wahariri wa vyombo vya habari ili watoe kipaumbele katika kuhamasisha wananchi
juu ya matumizi ya dawa za kukinga magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele
ambayo ni Matende na Mabusha, Usubi,Minyoo na Trakoma ili kuweza kutokomeza
kabisa ugonjwa huo hapa nchini.
Mkurugenzi
wa Blog ya Full Shangwe Bahati Bukuku akitoa mchango katika Semina ya
uhamasishaji juu ya magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele mbele ya wahariri
na wakuu wa Idara ya Afya.
Watumishi
wa Idara ya Afya wakifuatilia kwa makini Semina ya uhamasishaji wa magonjwa
yaliyokuwa hayapewi kipaumbele iliyofunguliwa na Mganga Mkuu wa Serikali Prof.
Bakar Kambi mapema leo katika ofisi za Wizara ya Afya jijini Dar es salaam.
No comments:
Post a Comment