Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Alhaj, majid Mwanga
amewataka waombaji wa nafasi za kujiunga na Jeshi la Kujenga Taifa JKT wilayani
humo, kuacha udanganyifu wa makazi ili
kutoa nafasi kwa wakazi halisi kupata nafasi hizo.
Mkuu huyo wa wilaya alitoa kauli hiyo wakati
wakufunga mashindano ya Mazingira Kabumbu Cup 2017 yaliyofanyika katika uwanja
wa Mwanakalenge Mjini Bagamoyo.
Alisema Rais wa Jmhuri ya Muungano wa Tanzania
Dkt. John magufuli ametoa nafasi katika kila wilaya ili kila mwananchi mkazi wa
wilaya husika apate nafasi hiyo hivyo si kutoka kwenye wilaya yako kuja kuomba
nafasi hizo kwenye wilaya ambayo wewe sio mkazi.
Alisema katika usaili unaotarajiwa kufanyika
Tarehe 15 Novemba mtu atakaebinika si mkazi wa wilaya ya Bagamoyo atakamatwa na
polisi na kuwekwa mahabusu kwa kuingilia makazi ambayo si yake ili hali nafasi
hizo zipo kila wilaya nchini kote.
Aidha, Mkuu huyo wa wilaya ya bagamoyo, alitumia
nafasi hiyo kutoa wito kwa wakazi wa wilaya ya Bagamoyo kujitokeza kuomba
nafasi hizo ambazo zipo kwa iwango tofauti vya Elimu.
Alisema nafas zilizopo ni 65 tu hivyo kila kata
inaweza kutoa vijana watakaojiunga na Jeshi la Kujenga Taifa.
Aliwataka wenyeviti wa vitongoji kutoa
ushirikiano katika hilo ili kuhakikisha vijana watakaoingia kwenye usaili wawe
ni vijana wa Bagamoyo.
No comments:
Post a Comment