Uongozi wa Yanga umesema hautaenda mahakamani kupinga Simba kupewa pointi
tatu.
Simba imeshinda rufaa yake dhidi ya Kagera Sugar na kupata pointi tatu na
mabao matatu ikiwa ni baada ya kubainika beki Mohamed Fakhi alicheza mechi
dhidi ya Simba akiwa na kadi tatu za njano.
Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Yanga, Salum Mkemi amesema kama kuna
wanachama wanataka kwenda mahakamani, wao hawatakuwa na uwezo wa kuwazuia huku
akisisitiza Tanzania ikifungiwa, Serengeti Boys itang’olewa kushiriki michuano ya
Kombe la Mataifa Afrika na ile kauli mbio ya Gabon mpaka Kombe la Dunia
itageuka na kuwa “Gabon hadi Nyumbani Tanzania”.
“Wakiendelea hivi itakuwa ni Gabon hadi Nyumbani, haitakuwa Kombe la
Dunia tena.
”Watu wana hasira zao, sisi viongozi tunaweza tusijue kinachoendelea.
Kagera ni timu ndogo, wanaonewa, hawatendewi haki. Sasa sisi tumeinunua hii
kesi.
“Ajabu kabisa, waamuzi wameitwa wawili tu na wengine hawakuitwa. Hii si
sawa, kuna jambo hapa,” alihoji Mkemi akionekana ni mwenye jazba.
No comments:
Post a Comment