Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Emil Malinzi
amezipa kongore timu za JKT Oljoro ya Arusha, Mawenzi ya Morogoro na Transit
Camp ya Shinyanga kwa kufanikiwa kupanda daraja baada ya kufanya vema kwenye
hatua ya Nne Bora (Play off) iliyofikia kikomo jana Aprili mosi, mwaka huu.
Katika salamu zake za pongezi, Rais Malinzi amezitaka timu hizo sasa
kujiimarisha katika nyanja za usajili na maandalizi mengine ili kuwa timu za
ushindani katika Ligi Daraja la Kwanza (FDL) ambako watashiriki kuanzia msimu
mpya utakaoanza Julai, mwaa huu.
“Nichukue nafasi hii kuzipongeza timu zote ambazo zimepanda daraja kutoka
Ligi Daraja la Pili na kwenda Ligi Daraja la Kwanza. Pongezi nyingi ziwaendee
wanafamilia wote kuanzia viongozi, wachezaji, waamuzi walioamua mechi zao,
mashabiki nakadhalika,” amesema Malinzi na kuongeza:
“Huu ni uthibitisho kuwa timu zote ziliajianda vya kutosha na kupata
matokeo,naamini hata Cosmopolitan nayo ilijiandaa lakini kwa bahati mbaya pointi
hazijatosha kwa msimu huu. Ni imani yangu kuwa itapambana msimu ujao na
kufanikiwa.”
Kadhalika Rais Malinzi alizitakia kila la kheri timu zote katika kumaliza
msimu na kuanza msimu ujao.
No comments:
Post a Comment